Tuesday, April 9, 2013

BABU WA LOLIONDO AANZA KAZI TENA KARIBU SAMUNGE

 

 
Mchungaji Ambilikile Mwasapila maarufu kama babu wa Loliondo anayetoa huduma ya dawa kwenye kikombe kwa imani inayodaiwa kutibu magonjwa sugu ya binadamu, ameibuka na kudai watu watarajie maajabu makubwa zaidi ambayo mungu amemuanesha hivi karibuni

Miongoni mwa maajabu hayo ni uwepo wa unyayo wa mtu wa 182 tangu kuumbwa kwa mwanadamu wa kwanza Adam, na kwamba bustani ya eden inayoaminika kuwa waliishi Adam na Eva ilikuwa Ngorongoro

Kilometa takribani 300 kutoka mjini Arusha,kamera ya kituo hiki inazuru eneo la Samunge Ngorongoro kukutana na Mchungaji Ambilikile Masapimla au Babu wa Loliondo

Kwa takribani miaka mitatu ya utoaji wa huduma ya Kikombe chenye dawa, ametokea kuwa mtu mwenye umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Akiwa na umri wa miaka 78 sasa umaarufu wa mchungaji masapila umelifanya eneo la Samunge katika wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha kuwa na umaarufu wa kipekee

No comments:

Post a Comment