MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Mario
Balotelli amefungiwa mechi tatu za Serie A baada ya kumbwatukia mshika
kibendera katika mechi dhidi ya Fiorentina juzi.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa
Manchester City, Balotelli tayari alikuwa amefungiwa moja kwa moja mechi
moja baada ya kupata kadi yake ya nne ya njano msimu huu katika mechi
hyo iliyoisha kwa sare ya 2-2.
Tulia wewe: Kipa wa Fiorentina, Emiliano
Viviano (katikati) akimtuliza Balotelli, wakati anamtupia maneno mshika
kibendera Daniele Doveri
Hata hivyo akaongezewa adhabu ya mechi mbili zaidi katika taarifa iliyotolewa leo kwa kosa la kumbwatukia mshika kibendera huyo.
Mshambuliaji huyo wa Italia ameifungia
mabao 10 klabu na timu yake ya taifa katika mechi 11 mwaka huu, lakini
atakosa mechi zijazo za Milan dhidi ya Napoli na Juventus sambamba na
Catania.
Kazini: Balotelli alisimama mbele wakati Milan inatoa sare ya 2-2, angalia hapa anavyochukua mpira wa juu
Balotelli akipambana
Milan inashika nafasi ya tatu Serie A,
ikizidiwa pointi nne na Napoli katika kinyang'anyiro cha nafasi ya pili,
huku Juventus ikiongoza kwa poinyi tisa zaidi.
Tukio hilo linakuja mara tu baada ya Balotelli kukutwa anavuta sigara chooni kwenye treni.
No comments:
Post a Comment