VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Yanga SC leo wamepunguzwa kasi baada ya
kulazimishwa sare tasa na wenyeji Polisi,
mchezo uliopigwa kwenye dimba la Jamhuri Mjini Morogoro.
Matokeo ya leo yameifanya
Yanga kutibua rekodi yake ya kushinda
mechi zake zote tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Katika mchezo huo, timu hizo ziliunza
mchezo kwa kusomanana ambapo Yanga ilipata kona dakika ya 13, 26, 31, 43 na
45 huku Polisi Moro ilipata kona katika dakika ya 10, 27,37 na 41.Kona zote hazikuzaa
matunda.
Katika dakika ya 24 amanusra
kiungo wa Mokili Rambo atiukise nyavu za Yanga kabla ya beki Mbuyu Twite kuokoa
mchomo huo ukiwa unaelekea nyavuni.
Aidha, Kipa wa Polisi, Kondo
Salum alifanya kazi ya ziada dakika ya 26 kupangua mpira wa kichwa wa beki wa Yanga,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kufuatia kona maridadi ya David Luhende.
Mshambuliaji wa Yanga, Said
Bahanuzi ‘Spider Man’ aliikosa bao la
wazi, baada ya kuchelewa kuiwahi krosi nzuri ya Simon Msuva na mpira
ukapitiliza hadi mikononi mwa kipa wa Polisi.Na hivyo kumaliza kipindi cha
kwanza kwa 0-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa
kila timu kusaka bao kwa udi na uvumba, huku
Polisi wakiutawala zaidi mchezo lakini walishindwa kuzitendea haki nafasi za
wazi walizozipata .
Katika dakika ya 51, Mbuyu Twite alipewa kadi ya njano baada
ya kupuuzia maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo Dominic Nyamisana kutoka Dodoma.
Yanga ilimtoa Nizar Khalfan,
Said Bahanuzi na kumuingiza Stephano Mwasika na Didier Kavumbagu, huku polisi
wakimtoa Mokili Rambo na kumuingiza Keneth Masumbuko.
Kwa matokeo hayo Yanga
imefikisha pointi 49, ikifuatiwa na Azam Fc yenye pointi 43 na Kagera Sugar ikiwa
ya tatu kwa pointi 37.
Yanga SC ; Ally Mustafa
‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan,
Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Said Bahanuzi/Didier
Kavumbangu , Hamisi Kiiza na Nizar Khalfan/Stefano Mwasyika dk46.
Polisi Moro; Kondo Salum,
Rodgres Freddy, Castro Ngwangila, Chacha
Marwa, Salmin Kiss, Nahoda Bakari, Bantu Admin, Muzamil Yassin, Mokili
Rambos/Kenneth Masumbuko dk 75, Machaku Salum na Nicholas Kabipe.
No comments:
Post a Comment