Saturday, March 30, 2013

BARABARA MAKETE HALI MBAYA



Mkuu wa wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro amewataka wananchi  wa makete  kushiriki ktk  ukarabati wa miundombinu ya barabara pindi tatizo linapotokea ktk maeneo korofi

Akizungumza ktk kipindi cha morning power kwa njia ya simu Bi.Matiro amesema wananchi wanatakiwa kuwa na ushirikiano pindi barabara zinapokuwa zimeharibika ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Makete

Hata hivyo amesema kuwa viongozi wa tanrods amewapa taarifa kuhusiana na tatizo hilo lililoko ktk maeneo MENGI HAPA WILAYNI MAKETE HASA KATIKA KIJIJI CHA IVALALILA ambapo magari ya kutoka Mbeya kuja makete yanashindwa kupita kulingana na ubovu wa barabara hiyo

Mtandao huu ulifika eneo la tukio nakujionea hali halisi ya ya marabara ambapo mpaka sasa hakuna mawasiliano kutoka Makete kwenda jijini mbeya kutokana na shimo lililopo eneo la Ivalalila ambapo mpaka sasa hali bado ni mbaya 
 Mtandao huu haukiishia hapo ulikwenda moja kwa moja kuongea na wamiliki wa vyombo vya usarishaji ambapo mmiliki wa kampuni ya Japanice Junich Daniel alimarufu kama  Mwarabu alisema "kwa hali hii inakoelekea usafiri wa Makete na Mbeya hautakuwepo kutokana na tunaingia gharama nyingi kufanya marekebisho ya magari kutokana na mara nyingi kugongesha katika mashimo ya barabarani"

Akiendelea Mwarabu alisema"natumia fursa hii kumuomba mbuge na uongozi mzima bila kumsahau waziri mwenye dhamana kuweza kutufanyia marekebisho katika barabara za wilaya ya makete kuwa hali tete hususani nyakati za masika 


No comments:

Post a Comment