Thursday, March 21, 2013

RIPOTI KAMILI YA FG BLOG KUHUSU UCHAKAVU WA BARABARA IRINGA



Hili ni  shimo lililopo eneo la Sambala mjini Iringa barabara  ya Iringa - Dodoma
Hapa ni  eneo la Kihesa  sokoni barabara ya Iringa - Dodoma
Kihesa mjini Iringa
Hapa ni Eneo la Makosa  mjini  Iringa karibu kabisa na ofisi  za Manispaa ya Iringa
RC Iringa Dkt Christina Ishengoma upo ?
  Meneja  wa TANROADS mkoa Paul Lyakurwa (kushoto ) akimpokea  waziri mkuu Mizengo Pinda ,wa kwanza  kushoto ni katibu  wa mbunge jimbo la Ismani Thom Malenga
Shimo eneo la Mwang'ingo mjini Iringa
Hapa si kijijini ni Iringa mjini
Kihesa  mjini Iringa na hii ni barabara ya mkoa  wa Iringa si kijiji ,inangoja  ziara ya viongozi wa kitaifa ndipo  itengenezwe
Barabara kibogoyo mjini Iringa umepata kuona ?
Hili  shimo  lipo nje ya ofisi ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kama kwa mwakilishi wetu ni hivi
 Hali  ya  barabara  ya  mkoa  wa  Iringa ,barabara ya  Iringa -Dodoma kuanzia eneo la Samora hadi Kihesa  kilolo katika  Manispaa ya  Iringa ambayo ni sura ya mkoa  wa Iringa ni mbaya na inayosikitisha na hata  kuchafua  mwonekano wa mkoa  wa Iringa kwa ujumla.
Yawezekana zipo  sababu  zinazopelekea  kuwepo kwa ubovu huo  wa barabara sababu ambazo uongozi  wa wakala wa barabara  mkoa  wa Iringa TANROADS unazijua ila yawezekana pia  sababu  hizo  hazikubaliki  kwa  watumiaji  wa barabara  hiyo hasa  ukizingatia  kuwa maeneo ambayo barabara  hiyo  imechakaa kupita kiasi ndio  sura ya mkoa mzima.
Binafsi imenichukua muda wa  zaidi ya miezi  miwili  sasa  kujiuliza maswali  mengi yasiyokuwa na majibu  kuhusu TANROADS  mkoa  wa Iringa  inavyofanya  kusudi  kuendelea  kuacha barabara  hii nyeti kwa sura ya mkoa  wetu  ikiendelea  kuharibika bila kuchukua hatua za  kuziba japo mapengo yanayoendelea  kuitesa barabara  hii ya Iringa - Dodoma katikati ya mji  wa Iringa.
Si wakati  wa kuwafundisha kazi  viongozi  wa TANROADS mkoa  wa Iringa  wala mwenyekiti  wa kamati ya  ulinzi  na usalama mkoa wa Iringa na mkuu  wangu  wa mkoa Dkt  Christina  Ishengoma kuhusu kero  hii ya barabara  ndani ya mji  wa Iringa.
Ila ni  wakati  wa  kuwaomba viongozi  wangu hawa kwa maana ya wakala wa barabara  mkoa  wa Iringa Injinia Msomi Paul Lyakurwa ambae ni meneja wa TANROADS mkoa  wa Iringa , mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia  Warioba na mkuu  wangu  wa mkoa Dkt Ishengoma  kutoka ofisini na kusaidia  msaada  wa meno  kwa kibogoyo huyu barabara ya Iringa - Dodoma.
Zamani  nilikuwa  nikishuhudia  wananchi  wa vijijini  ndio ambao  walikuwa  wakilalamikia ubovu wa barabara  ila  leo katika karne hii ya sayansi na Teknolojia tunashuhudia mapengo ya  barabara  yanatesa mjini ambako  viongozi  wote wapo.
Binafsi siamini kama ajali zinazotokea katika mji  wa Iringa  zinasababishwa na uzembe  wa madereva ila ninachoamini ajali  hizi zinasababishwa na uwajibikaji mbovu  wa wenye mamlaka  waliopewa kusimamia  barabara hii na hata  kuacha barabara  kuwa na mashimo makubwa kama haya .
Barabara   za mji  wa Iringa ni chakavu  sana na mbaya zaidi kwa sasa  ubovu huo  umesogea hadi katika  ofisi ya  mbunge Mchungaji Peter Msigwa ambae ni mwakilishi  wa  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini ila pia  bila aibu mashimo  yamesogea hadi katika mlango  wa  mkuu  wa mkoa  wa Iringa ambapo katika lango lake  kuna mashimo ambayo naweza kusema ni mashimo ya karibu  wageni ofisi ya RC Iringa.
Mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com wakati ukiandaa ripoti  hii   ulitaka  kupita  barabara ya Pawaga  Road  ili kuona  barabara ya mbunge na mkuu wa mkoa ikoje na kuona pia kuna shida .
Haya  ni maeneo ambayo  yameathirika  kupita kiasi na bila  shaka  uongozi wa barabara  mkoa wa Iringa unasubiri ziara ya  viongozi wa kitaifa  ili  kufanya kazi usiku na machana kuziba mashimo haya ambayo kweli yanaifanya  serikali iliyopo madarakani  kuendelea  kuchukiwa zaidi na wapiga  kura  wake achiliambali mbunge wa jimbo ambae yeye ni mkazi  wa Iringa na anashuhudia ubovu huu.
Uchunguzi unaonyesha kuwa eneo la Nationali mjini Iringa limeharibika  vibaya , eneo la Zebra ,eneo la Tanesco , eneo la ofisi ya mbunge wa Iringa mjini ,eneo la ofisi ya RC Iringa , eneo la Makosa , TFA , Sabasaba , Sambala , FFU, Kihesa na Mwang'ingo ndio ambayo ni hatari zaidi kwa  usalama  wa watumiaji wa vyombo vya moto kwani mashimo ni makubwa zaidi na iwapo hatua  za haraka hazitachukuliwa ajali katika  mji wa Iringa si chanzo cha madereva bali ni uzembe  wa TANROADS kushindwa  kuchukua hatua  zaidi .
Zipo  sababu  kuwa eti barabara   hiyo inatengenezwa na  wachina  kutoka Iringa - Dodoma  ila kasi yake ni ndogo  zaidi na hata kama hivyo bado  wakati  tunasubiri ujenzi huo ni vema ukarabati uwepo.
...........................................ITAENDELEA  WIKI IJAYO 

No comments:

Post a Comment