TAKUKURU MBEYA WAMNASA MWALIMU KWA RUSHWA YA SH.200 KUTOKA KWA WANAFUNZI
MWALIMU Faustin wa shule ya sekondari ya
Forest iliyopo Jijini Mbeya amejikuta akitiwa mbaroni baada ya muda
mrefu kuwaomba na kupokea rushwa ya Sh.200 kutoka kwa wanafunzi wake
wanaochelewa na kuvaa viatu ambavyo havina kamba.
Arobaini za mwalimu huyo zilitimia jana baada ya maafisa wa Takukuru mkoa wa Mbeya kuinyaka issue hiyo na kutege mtego uliofanikisha kumnasa mwalimu huyo kinara wa rushwa shuleni hapo.
Mwalimu huyo alikutwa na maafisa wa Takukuru akiwa tayari amekusanya kiasi cha Sh.64,000 huku msaidizi wa ulaji rushwa hiyo Mwalimu Mwasote akifanikiwa kuwazidi mbio maafisa wa Takukuru kisha kutokomea kusikojulikana.
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na kikosi kazi cha mtandao huu shuleni hapo walisema kuwa wamefurahishwa na Takukuru kumkamata mwalimu huyo mwenye urefu usiozidi futi taano na nusu huku akiwa na kitambi.
Walisema kuwa mwalimu huyo licha ya kuwatoza Sh.200 wanafunzi wanaochelewa au kuwa na makosa mbalimbali shuleni hapo, pia alikuwa akiwavua viatu wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kununua viatu vya kamba na kuwatoza kati ya Sh.500-2000 endapo wanafunzi wakishindwa kumpa rushwa hivyo alikuwa akivipeleka viatu vyao kwenye matanuru ya matofali ili kuwashia moto.
Sanjari na hayo mwalimu Faustine, anatuhumiwa na wanafunzi kuwatesa kwa kuwainamisha miguu juu kichwa chini bila kujali jinsia zao wala mavazi na ambao wanashindwa anawaambia watoe Sh.200 na kwamba ofisi ya walimu inaitwa Gwantanamo!
Shule hiyo ni ile ambayo Mkuu wa shule ambaye ni mwanamke aliwahi kuwaambia wazazi kuwa watoto wao wa kike wote ni wake za watu baada ya kuwapima na kutofanikia kumkuta hata mmoja na usichana wake.

No comments:
Post a Comment