Tuesday, March 5, 2013

MWILI WA ALIYEZAMA KTK BWAWA LA TANWATT KIBENA NJOMBE WAONEKANA LEO NA KUZIKWA

 Hapa wakifanikiwa kuokoa mwili wa kijana Mexon Chota aliyekuwa msanii wa Kikundi cha KIBENA ARTS GROUP.
 Mwili wa Kijana aliyezama kwenye moja la Bwawa la TANWATT Kibena Mkoani Njombe tangu siku ya Ijumaa Jioni wiki iliyopita ukionekana hapa.
 Hapa kichwa cha marehemu kikionekana baada ya kuokolewa wakati wakivuta.
 Baada ya mwili wa marehemu kuokolewa leo na wataalamu wa uokoaji toka mkoani Iringa.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mexon Chota Mahali pema peponi Ameeeen,
 
Mazishi ya Mkazi Mmoja wa Kibena Mjini Njombe Mexon Nyekelela Chota

Yamefanyika Leo Katika Makaburi ya Kibena kanisa la roman ya zaman,Ikiwa ni Baada ya Kupatikana Kwa Mwili wa Marehemu Uliokuwa umezama Kwa Siku ya Tano Katika Mabwawa ya Kampuni ya TANWAT Mjini Njombe.

Mwili wa Marehemu Ulipatikana Leo Majira ya Saa Nane Mchana Ikiwa ni Baada

ya Jitihada za Muda Mrefu za Wananchi na Viongozi Kuweza Kuutafuta Mwili Huo

Bila Mafanikio Kutokana na Ukosefu wa Vifaa Vya Uokozi.

Akizungumza Mara Baada ya Kupatikana Kwa Mwili Huo Afisa Tarafa ya Njombe

Mjini Bi Lilian Nyemele Ameishukuru Kampuni ya TANWAT Kwa Namna

Ilivyoshiriki Katika Kusaidia Zoezi Hilo Pamoja na Wananchi Wote Walioshiriki.

Akizungumza Mara Baada ya Kuwasili Mkoani Njombe Mtaalam wa Uzamiaji

Kutoka Jijini Dar Joseph Mapunda Anasema Kuna Haja Kwa Serikali ya Mkoa wa

Njombe Kuanza Kutoa Mafunzo Kwa Wananchi na Wataalam Mbalimbali Ili

Kuweza Kupata Wataalam wa Uzamiaji.

Marehemu Mexon Nyekelela Chota Alizama Kwenye Mabwawa Hayo Mnamo

March Mosi Mwaka Huu Majira ya Saa Kumi na Moja Jioni Wakati Akiwa na

Wenzake Mara Baada ya Kumaliza Shughuli Zao za Sanaa.

viongozi wa mitaa ya kibena Faustin Mwenda na Pasval Kaduna wanazungumza

mara baada ya mazishi hayo

Mama wa marehemu Mexon Chota kwa masikitiko makubwa nae akatoa neno

No comments:

Post a Comment