Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amejitoa kwenye Tume ya serikali kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha kustisha cha matokeo ya kidato cha nne, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amejitoa kwenye Tume ya serikali kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha kustisha cha matokeo ya kidato cha nne, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mbatia ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wajumbe wa
tume hiyo yenye wajumbe 15, alisema kamwe hatoweza kufanya kazi yake
kwa uhuru kwa sababu ni Mbunge wa kuteuliwa, kamati hiyo imeundwa na
serikali hivyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.
Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya chama hicho
kumwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kikimuomba aunde tume ya kudumu
ya elimu nchini.
Tume hiyo iliundwa kutokana na matokeo mabaya ya
mtihani wa kidato cha nne, watahiniwa 240,903 kati ya 480,036
waliofanya mtihani walipata alama sifuri, huku 23,520 sawa na asilimia
5.16 wakifaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakipata daraja
la nne.
Januari 31, mwaka huu katika kikao cha bunge,
Mbatia aliwasilisha hoja binafsi kuhusu udhaifu katika sekta ya elimu
akielezea kwa kina, sera ya elimu iliyopitwa na wakati, kukosekana kwa
mitalaa, kuwapo kwa mihtasari mibovu ya masomo na vitabu kuwa na viwango
duni.
Hata hivyo, wabunge wa CCM wakishirikiana na Serikali walimaliza hoja hiyo bila kutolewa majibu ya msingi.
Mbatia alisema jana kuwa hawezi kufanya kazi yake
kwa ufanisi ndani ya tume hiyo, kwa sababu ndiye aliwasilisha hoja
binafsi bungeni kuhusu udhaifu sekta ya elimu, hoja ambayo ilizimwa
bila kutolewa majibu ya msingi.
“Kamati ya Waziri mkuu haina jipya la kufanya kwa
sababu ipo Kamati iliyoundwa mwaka 2011 kuchunguza matokeo mabaya ya
kidato cha nne, imeeleza kila kitu na ripoti ipo ofisi ya waziri mkuu,
sasa hii ya sasa inakwenda kuchunguza nini?” alihoji Mbatia.
No comments:
Post a Comment