Sir Alex Ferguson alimuanzishia benchi
Wayne Rooney, lakini wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao mapema
kipindi cha pili, baada ya Sergio Ramos kujifunga.
Lakini mambo yaliwaharibikia baadaye
kidogo tu Man United, baada ya Luis Nani kuonyeshwa kadi nyekundu ya
moja kwa moja kwa kumchezea rafu Alvaro Arbeloa.
Na baada ya hapo, bao la Luka Modric
lilifuatiwa na bao la Ronaldo dakika tatu baadaye, hivyo vigogo hao wa
Hispania kutinga Robo Fainali.
VIKOSI, WAFUNGAJI...
Man United: De Gea, Da Silva (Valencia 87), Vidic, Ferdinand, Evra, Carrick, Cleverley (Rooney 73), Nani, Welbeck (Young 80), Giggs, van Persie.
Benchi: Lindegaard, Evans, Hernandez, Kagawa.
Kadi za njano: Evra, Carrick
Kadi nyekundu: Nani dk57.
Mfungaji: Ramos (Kujifunga) dk48.
Real Madrid: Diego Lopez, Arbeloa (Modric 59), Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso, Di Maria (Kaka 42), Ozil (Pepe 71), Ronaldo,Higuain.
Benchi: Adan, Benzema, Albiol, Callejon.
Kadi za Njano: Arbeloa, Pepe
Wafungaji: Modric dk67, Ronaldo dk69.
Refa: Cuneyt Cakir (Uturuki)
Mahudhurio: 74,959

Mshindi wa mechi: Bao la Ronaldo limeitoa timu yake ya zamani

Kiungo wa zamani wa Spurs, Modric akifunga bao la kusawazisha


Nje; Ronaldo akifunga bao lililoitupa nje United


Beki wa Real akijifunga


Kadi nyekundu: Hapa ndipo ilipofia United baada ya kupungukiwa mchezaji mmoja


Akitokea benchi: Rooney akipasha kutokea benchi


Welbeck alikaribia kufunga leo, lakini alikuwa ameotea


Vidic alipiga kichwa kikagonga mwamba kipindi cha kwanza


Giggs amecheza mechi ya 1,000 leo Man United


Ronaldo amepata mapokezi mazuri leo Old Trafford

Ronaldo alikuwa katika wakati mzuri leoOld Trafford

Ronaldo akipasua Old Trafford

Ronaldo alicheza kwa raha leo
No comments:
Post a Comment