Friday, March 29, 2013

JENGO LA GHOLOFA 16 LAANGUKA DAR

Jiji la Dar es Salaam limegubikwa na simanzi nzito kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Ghandi leo asubuhi.
Ajali hii mbaya imesababisha vifo vya watu 2 na kuacha idadi isiyofahamika, wakiwemo wajenzi na wapita njia, wakiwa wamekwama ndani ya kifusi.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova amewaambia waandishi wetu kuwa waokoaji wamefanikiwa kunusuru watu 15 wakiwa hai.
Taarifa zilizotufikia zinaongeza kuwa magari matatu yameteketea baada ya kuangukiwa na masalia ya jengo hilo, lililokuwa likijengwa na kampuni ya Lucky Construction Limited.
Katika harakati za kuhamasisha shughuli za uokoaji, Rais Jakaya Kikwete, Mwananchi imeelezwa, amewasili katika eneo la tukio.
Hata hivyo, kuna taarifa kuwa shughuli za uokoaji zinakwamishwa na vifaa duni, pamoja na jitihada za ziada kutoka kwa maofisa wa jiji wakishirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa na kampuni binafsi ya ulinzi ya Ultimate Security.

No comments:

Post a Comment