Friday, March 29, 2013

WANAFUNZI UKWAMA WAPATA VYOO




mkuu wa shule ya msingi Ukwama wilayani Makete Ebayoti Amani Malila ametoa shukurani za dhati kwa kupokea mradi wa ujenzi wa vioo katika shule yake mradi huo umetorewa na  AMREF 
 akizungumza na wanahari shuleni hapo katika wakati wa ukaguzi wa mradi huo bwana  Malila amesema amepokea kwa furaha kubwa  sana  kwani amewatoa  katika  hali mbaya ya kiafya  sasa wanaelekea  hali nzuri kiafya  ambapo huko nyuma walikuwa na vyoo ambavyo wanafunzi walikuwa wakijitegemea  kuchota maji ya kutumia katika  vyoo hivyo  lakini  wanashukuru  mradi huu ukikamilika .
akiendelea Malila amesema kuwa watoto watapata huduma nzuri ya choo 
kwani  maji yamejengewa ndani kwa ndani na watanawa maji yanayotiririka  kwenye Bomba hata hivyo aliongeza  mradi huu umejari  hata watoto  waremavu  na vilevile  uwapo  wa maji  chooni  tofauti na kuchota  na kwenda nayo chooni  na hali ya mlipuko wa magonjwa utapungua kutokana wanafunzi kula kinyesi kibichi kutokana nakushika vyombo vya chooni kwakukosa maji tiririka chooni. 
Pia ameongeza kuwa idadi ya watoto na kubwa kuliko vyoo vilivyojengwa kwani vinahitajika nyoo 15 na vilivyojengwa Mashimo 9 hivyo upungufu mashimo 6 kwa vyoo bora vya kisasa tunategemea  kwamba kama  shirika la AMREF litawasaidia tena liwajengee matundu  6 watashukuru sana. PICHA

 kwaupande wake mwalimu WINFRIDA MALUNGU amesema mradi huu  umepokea  kwa mikono  miwili na umewakomboa  sana ,kutoka vyoo vya shimo na kwenda kisasa inasaidia  wanafunzi  kwenda  na wakati pia  kuwaepusha na magonjwa  mabilimbali  kama Vichocho, na Kuhara na  matumbo.
Nae  Mwanafunzi SAMSONI KENETJ SANGA amesema vyoo vya zamani  vilikuwa ni vya shimo  na havikuwezesha  walemavu  kupata huduma hiyo kiurahisi. Wanashukuru  AMREF  kwa msaada huo  na wanaahidi  kutunza vizuri PICHA

M/kiti

  akimalizia kushukuru mwenyekiti wa kijiji hicho bwana NEHEMIA SANGA anashukuru AMREF  na ushiriki wa wananchi  kwa kupokea  na kujenga  mradi  huo Shuleni hapo pia  ameongeza kuwa mradi huo utapunguza usumbufu  wa kila mwaka  kuchimba shimo  kwani kwa muda mfupi  yalikuwa yanatitia .Hivyo  sasa  maendeleo yataongezeka  kwa kwakukombolewa /kujengewa  vyoo bora na AMREF.PICHA

 Mradi huo ambao unajengwa katika shule hiyo kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kupata huduma bora ya choo ili kukinga na magonjwa ya miripuko ambapo mradi huo unadhaminiwa na AMREF kwa kushirikiana na wana nchi kwani shirika hilo hutoa vifaa huku wananchi wakichangia katika nguvu

No comments:

Post a Comment