Katibu mkuu wa Njombe Pres Club Hamiss Hassan Kassapa nae akitamka neno baada ya kupita kwenye kinyang'anyiro cha uongozi nafasi ya katibu mkuu.
Msimamizi wa uchaguzi wa viongozi wa chama cha waandishi mkoa wa Njombe Fredrick Siwale.
Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe NPC jana Kimefanya Uchaguzi Rasmi na Kuwapata Viongozi wa Chama Hicho Watakao Kiongoza Kwa Miaka Mitatu Huku Wajumbe wa Chama Hicho Wakimchagua Merce James Kuwa Mwenyekiti wa NPC Huku Hamiss Hassan Kassapa Akichaguliwa Kuwa Katibu mkuu.
Katika Uchaguzi Huo Nafasi Mbalimbali Zimegombewa Ikiwemo Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Iliyochukuliwa na Elymethew Kika , Lilian Mkusa Akichaguliwa Kuwa Naibu Katibu , Nafisi ya Mtunza Hazina Imechukuliwa na Sunday Bavuga Huku Gabriel Kilamlya Amechaguliwa Kuwa Mtunza Hazina Msaidizi.
Uchaguzi Huo Ulisimamiwa na Bwana James Siwale na Shaban Lupimo Kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa IPC Wamesema Uchaguzi Huo Umefanyika Kwa Haki na Demokrasia , Ambapo Msimamizi Mkuu James Siwale Wametangaza Matokeo ya Uchaguzi Huo.
Pia Chama Hicho Kimewachagua Wajumbe Saba wa Kamati Tendaji Ambao Wanaungana na Viongozi Sita wa Ngazi za Juu Kuunda Timu ya Wajumbe 13 wa Kamati Hiyo Inayoongozwa na Merce James na Hamis Kasapa Kama Anavyoeleza Msimamizi Masaidizi wa Uchaguzi Bwana Shaban Lupimo
Kabla ya Uchaguzi Huo Viongozi wa Mpito Walijiuzulu Nyadhifa Zao na Kuwashukuru Wanachama wa NPC , Ambapo Viongozi Wapya Waliochaguliwa Wamewashukuru Wajumbe wa Chama Hicho na Kuwaomba Kuendeleza Mshikamano Ili Kufanikisha Malengo ya NPC,
Uchaguzi Huo Unafanyika Baada ya Kukamilika kwa Usajili wa Chama Hicho Chini ya Uongozi wa Muda Pamoja na Agizo Kutoka Umoja wa Vyama Vya Waandishi wa Habari Nchini UTPC la Kuitaka NPC Kuwasilisha Mihtasari ya Vikao , Majina ya Viongozi Pamoja na Wanachama Wanaotambulika Kisheria.
Bodi ya uongozi huo imeundwa na wajumbe 13 ambao watahakikisha wanashirikiana na viongozi waliochaguliwa kusimamia na kutetea haki za waandishi ikiwemo kuhoji uhalali wa kuendelea matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na viongozi wengine wa serikali. picha na RIZIKI MGAYA
No comments:
Post a Comment