Wednesday, March 27, 2013

BIBI MIAKA 60 ABOMOLEWA NYUMBA MNA ANUSUSURIKA KUFA KWA TUHUMA ZA UCHAWI RAFIKI YAKE CHUPUCHUPU POLISI WAMUOKOA

Wananchi wenye hasira kali wakianza kuvunja nyumba ya Bibi Huyo
anaedhaniwa ni mchawi...!

Bibi Huyo mwenye Umri wa Miaka (60) aishie kata ya masewe
wilayani Ilemi Mkoani Mbeya...Jana alinusurika kifo Baada
ya wananchi wenye Hasira kali kuchoshwa na Vitendo vya
Kichawi vinavyoendelea kijijini hapo na Bibi huyo akiusishwa..



Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa mtaani hapo kwa
 ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtoto lakini Mwanamke
 huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu
 miongoni mwa wakazi hao hali iliyopelekea kuhisiwa
kuhusika na tukio hilo.


 
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23 Mwaka huu
 majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea
 kusisitiza kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa
 kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa mototo ambapo
 iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.


Mtoto wa Bibi Atukipile akiokoa vitu kadhaa vilivyosalia...!!
 
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na kufanya upekuzi
 walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina
 ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo
Mwanamke huyo baada ya kuulizwa alishindwa kutolea
ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na hasira
na kuanza kumpiga.
 
Kutokana na tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa huo Nedy
 Mwamlima alimnusuru Mwanamke huyo katika kipigo
 kutoka kwa wananchi kwa kumpeleka katika kituo kikuu
cha Polisi kwa usalama zaidi.
 
Baada ya mtuhumiwa huyo kunusuriwa na kukimbizwa
 katika kituo cha Polisi wananchi hao hawakupoza jazba
 zao ambapo waliamua kuteketeza nyumba ya mtuhumiwa
ikiwa ni pamoja na kufyeka mazao yaliyokuwa yamepandwa
 jirani na nyumba yake.
Hata hivyo hasira za wananchi hao hazikuishia hapo bali
walimsakama Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la
Agnes Sika ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la Pentecost
 Groly  kwa madai kuwa ni rafiki wa mtuhumiwa na amekuwa
akimfichia siri.


 
Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo laTukio na kumnusuru
Agnes asipatwe na madhara ikiwa ni pamoja na kutochomewa
 nyumba yake ambayo tayari wananchi hao walionekana
kuikimbilia kwa ajili ya kutaka kuibomoa.


 
Aidha Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa
 kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na upelezi ambapo Baba
 mzazi wa Mtoto anayesadikiwa kupotea katika Mazingira ya
 kutatanisha akisema anamwachia Mungu  baada ya juhudi
 za kumtafuta kushindikana.
Bibi Atupele pembeni akiwa na Mjukuu wake kwenye picha
ya Pamoja...Bibi huyo anaedhaniwa Mchawi
Baada ya vitendo vya kichawi kukithiri kijijini hapo....
Ni Baada ya Mtoto wa Miaka 11 kupotea Ghafla baada tu
ya kuena kumsalimia Bibi huyo Nyumbani kwake Majira ya
Ya Saa 11 Jioni.....!!

No comments:

Post a Comment