Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
ametembelea eneo la tukio ambapo jengo la ghorofa kumi lilianguka leo asubuhi
na kuua watu wawili huku wengine kadhaa wakihofiwa kunasa kwenye kifusi.
Kwa mujibu wa vikosi vya uokoaji watu kumi na tano pekee ndio waliofanikiwa kuokolewa wakiwa hai.
Jengo hilo
liliangua maajira ya sambili na dakika arobaini na tano ambapo watu wengi
walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida kabla ya kusikika kishindo
kikubwa kilichotokana na kuanguka kwa ghorofa hilo.
Kamanda wa
kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amethibitisha kufa kwa watu
wawili kwenye ajali hiyo huku akisema ni watu kumi na tano pekee ndio
wameokolewa wakiwa hai na kuongeza kuwa huenda kunawengine wamenaswa kwenye
kifusi.
Vikosi vya
uokoaji vinaendelea na juhudi za kuwaokoa watu wanaoelezwa kunaswa kwenye jengo
hilo ingawa hakuna idadi rasmi ya watu ambao wanaelezwa pengine huenda walikuwa
kwenye jengo hilo wakati linaanguka.
Mashuhuda wa
tukio hilo wamesema kuwa huenda kukawa na watoto ambao wamenaswa kwenye kufusi
kwakuwa wakati linaanguka walikuwa wakicheza jirani na jengo hilo.
Mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Sadick amesema kuwa uchunguzi tayari umeanza
kubaini chanzo cha kuanguka kwa ghorofa hilo na kwamba watu kadhaa wanahojiwa
ambao ni wahusika waliokuwa wakisimamia ujenzi wake.
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam,Mh. Mh. Said Meck Sadick akipatiwa maelezo ya namna ya uokoaji
kutoka kwa maafisa wa kikosi cha Uokoaji,Lakini Wanajitahidi lakini
wanakwamishwa na vifaa.
|
Wadau
wakionyesha nondo zilizokuwa zimejengewa kwenye jengo hilo wakimaanisha kuwa
hazina ubora.
|
Ulinzi
mkali.
|
KAULI YA MEYA WA ILALA KUHUSU GOROFA LILILOPOROMOKA
LEO DAR ES SALAAM LEO MARCH 29,2013.
No comments:
Post a Comment