Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Makete limeanza kujadili utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo katika ngazi ya kata ,kwa mwaka wa fedha 2012/13 wilayani hapa
Akifungua baraza hilo mwenyekiti wa madiwani Mh.Danieli Okoka amesema kuwa kila diwani anawajibu wa kuandaa na kutoa taarifa kwa wananchi wake
Kwa upande wa mwakilishi wa kata ya Tandala diwani wa Lupalilo Mh Manase amesema kuwa kata hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi kama wenye viti wa vijiji vya Ihela na Ikonda ,Bibi afya pamoja na mtendaji wa kata ya ikonda
Aida diwani wa kata ya itundu Mwinuka amesema kuwa kata yake inakabiliwa na upungufu wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea za kupandia na kukuzia
Jumla ya kata 22 kupitia madiwani wamewakilisha taarifa za utekelezaji i wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2012/2013.Huku changamoto kubwa ikiwa ni upungufu wa watendaji wa kata na vijiji
habari zaidi zitakujia
No comments:
Post a Comment