Tuesday, February 26, 2013

MAMA MJAMMZITO AJIFUNGULIA KWA JIRANI

 MWANAMKE mmoja amejikuta      akijifungua nje ya nyumba ya jirani yake ambako alikwenda kwa lengo la kuomba ushauri kuhusiana na ujauzito alioenda nao hapo

Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa juma lililopita maeneo ya Vingunguti Spenco jijini Dar es salaam.

Tukio hilo lilitokea majira ya usiku wa saa 7 na kushuhudiwa na mwandishi wa habari hii ambaye alikuwepo eneo la tukio hilo

Mwanamke huyo alifika nyumbani kwa jirani yake huyo aliyetambulika kwa jina la mama Happy majira ya saa 7 kasoro ili kuja kuomba ushauri kulingana na tatizo alilokuwa nalo

Maelezo ya awali aliyokuja nayo mwanamke huyo akiwa ameongozana na bwana wake huku wakiwa na mfuko aina ya Rambo yalidai kuwa, walikuwa wametokea hospitali kwa ajili ya kwenda kujifungua lakini wauguzi wa hospitalini hapo walimuamuru arudi nyumbani kwake kwa kuwa uchungu wa kuzaa mtoto ulikuwa bado haujafikia kiwango kinachotakiwa

Hivyo kwa mujibu wa maelezo yake alidai kuwa, wakati akiwa anaelezwa hivyo na wauguzi hao alidai yeye alikuwa akisumbuliwa na uchungu ambao aliona alikuwa ameshafikia hatua ya kujifungua lakini kwa maelezo yake aliamua arudi nyumbani pasipo na mabishano na wauguzi hao

Maelezo ya mwanamke huyo yanaendelea alidai kuwa, wakati wakiwa wanarudi nyumbani na bwana wake huyo walipata wazo wapitie kwanza kwa jirani yao huyo mtaa wa tatu kutoka nyumba wanayoishi

Ndipo usiku huo walithubutu kupiga hodi na wenyeji walipotoka kuwasikiliza shida yao alianza kumpa maelezo hayo kabla mwenyeji huyo hajawajibu wala kuwapa ushauri ndipo mama huyo alipojinyoosha na kuanza dalili zote za kusukuma na hatimaye akajifungua uani mwa nyumba hiyo na kuleta mayowe kwa mwenyeji huyo kuhaha huko na huko kuomba msaada kwa wanawake wenzake waishio karibu nae

Hali hiyo iliwashitua wengi baadhi ya akina mama waliitikia wito na kumkuta dada huyo akiwa chini huku kitoto kikiwa kinalia, msaada wa karibu ukahitajika na kwenda kuitwa mwanamke mmoja ambae alikuwa akiishia hatua na hapo aje kuwasaidia kwani yeye alikuwa na taaluma ya ukunga

Hata hivyo wakati mwanamke huyo akiwa bado hajamalizia hatua zingine za kujifungua nesi huyo alimuamuru mwanamke huyo atoe kadi lake la kliniki na alionyesha mfuko na kupekua ndipo wakakuta kadi hilo ambalo lilikuwa na mapungufu na mkunga huyo akawaambia baadhi ya akina mama waliokuwepo hapo kwamba hataweza kuendelea na kazi hiyo kwa kuwa mwanamke huyo alihudhuria kliniki siku moja tu na hakuwahi kupima hata kipimo kimoja cha maradhi ambayo ni muhimu kwa kila mwanamke mjamzito apime ili kuweza kumtambua

Hali hiyo iliwashangaza walio wengi hata waliokuwa wakitaka kumsaidia wakasogea pembeni kutokana na mama huyo afya yake ilikuwa haitambuliki kwa wakati huo huku mtoto akiwa analia wakati akiwa hajatenganishwa na mama yake

Hali hiyo ilichukua zaidi ya dakika 45 mtoto huyo akiendelea kulia akiwa chini michangani bila kupata ufumbuzi jinsi gani wamsaidie Hata hivyo baadhi ya wasamaria walijitolea kumsaidia mwanamke huyo hivyohivyo ili kunusuru uhai wa mtoto na alipotakiwa atoe vifaa vya kujifungulia mwanamke huyo alidai hana na hakuwa na kifaa cha aina yoyote na alipotakiwa atoe hata gloves wamsaidie navy o alijibu hakuwa nazo hali hiyo ndiyo ikazidi kuwaumiza vichwa akina mama waliokuwa mahali hapo

Unaweza ukadhani ni hadithi ama historia mama mmoja alichoshwa na hali hiyo alichukua uamuzi wa kuokota mfuko wa Rambo ulioukuwa karibu naye na kuokota kipande cha chupa, huku mwingine aliokota kipande cha wembe alichokiona mbele yake ndipo wakaendelea kumsaidia mwanamke huyo na waliweza kufanikiwa na baadae alibebwa kupelekwa hospitalini

Wasamaria waliokuwa mahali hapo wakagundua mwanamke huyo alipofika hospitalini wauguzi walimfukuza kutokana na kukosa vifaa hivyo na sababu ingine iliyopelekea afukuzwe ni kutohudhuria kliniki ama hajafika kabisa hospitali na alitumia uongo kuongopa kwamba aliambiwa arudi nyumbani ili aweze kusaidiwa

Mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kiume aliyedaiwa kuwa na uzito wa kilo 4 kwa taarifa zilizorudi na wasamaria mara baada ya kumfikisha hospitali

No comments:

Post a Comment