Tuesday, February 12, 2013

MWENDESHA BODA BODA AVUNJIKA MGUU ADAI NI AJALI YA BAISKELI


Mwendesha  boda  boda katika  kijiji  cha Kitimbuka wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Doto Chusi akisaidiwa na  wasamaria wema katika Hospitali ya mkoa  wa Iringa  usiku  wa  leo baada ya kuvunjika mguu  wake katika ajali ya Boda boda huku mwenyewe na ndugu  wakidai kuwa ni ajali ya Baiskeli.

Imekuwa ni kawaida  kwa  waendesha Boda  boda kudanganya  juu ya chanzo cha ajali  zao  ili  kukwepa  kuwajibishwa  kutokana na wengi  wao  kuendesha vyombo  hivyo  bila kuwa na leseni  hivyo  hulazimika  kudanganya  kuwa ni ajali ya Baiskeli ama wameanguka wakati  wakifanya mazoezi ya  kumbimbia ama  wamepigwa na ng'ombe .n.k

No comments:

Post a Comment