Tuesday, February 12, 2013

KIJANA ANYWAY SUMU BAADA YA KUNYIMWA PENZI NA DENTI


kijana Kevini Swale akiwa amepoteza  fahamu baada ya  kunywa  sumu ,huku mkononi akiwa ameshika pipi ya upendo kwa mpenzi  wake ,pembeni  kukiwa na ujumbe aliotaka kuuacha ,sumu ya panya na maji
Wananchi  wakimtazama  kijana  huyo aliyezima kwa  kunywa sumu kisha kunyimwa penzi
Hapa kijana  Kevini akinywa dripu baada ya  kufikishwa  Hospitali
Afande Stivine Nyatongo akiichunguza sumu  hiyo ,huku mkononi akiwa ameshika daftari lenye  ujumbe  mbali mbali 
Huu ndio  ujumbe  mbali mbali  aliouandika katika  kurasa zaidi ya 16
TUNU Siamini kama  wewe leo ndio chanzo cha  kifo changu kwani yako maneno matamu uliyokuwa ukinipa wakati  upo Tanga?
Haya na maandishi aliyojiandika mkononi yanasomeka TUNU WEWE NDIO CHANZO CHA KIFO CHANGU NAKUFA  ILI UJUE NAKUPENDA

UPO usemi  usemao kuwa mapenzi ni sumu na mapenzi  yanaua ni usemi ambao  ni vigumu  kuuelewa  ila ni rahisi  sana kuutumia usemi  huu kama ni funzo kwa wasiojua nini maana ya mapenzi.


Kwa  wakazi  wa  eneo la Pawaga Road mjini Iringa  usiku  huu wamepata  kuhusudia tikio la aina yake kutoka kwa kijana Kevin Swale (20) mkazi  wa Njombe ambae amelazimika  kunywa  sumu kwa  lengo la kujiua baada ya kunyimwa penzi na msichana mmoja mkazi  wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina la Tunu ambae  pia ni mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne mwaka jana.

Tukio hili la aina yake  kuelekea  siku ya  wapendanao duniani  limetokea leo jumanne mida ya saa 4 usiku katika eneo la barabara ya  Pawaga Road jirani na ofisi  za shirika la Nyumba Tanzania.

Mashuhuda wa  tukio   hilo  waliueleza mtandao  huu wa  www.rizikimgaya.blogspot.com  uliofika eneo la  tukio kuwa kijana huyo alikutwa akiwa hajitambui huku akiwa amelala katika mtaro  wa maji machafu na mkononi akiwa ameshika  pipi ya kijiti yenye  rangi  nyekundu mithiri ya siku ya  wapendanao   huku akiwa na  sumu  ya Panya na machi nyenye rangi ya  kijani ambayo yalikuwemo katika chupa za maji ya kunywa ambayo kwa kawaida huuza kati ya Tsh 500 hadi 600.


Mbali ya  kukutwa na sumu na maji hayo ambayo  pia yanasadikika kuwa ni sumu pia kijana huyo alikuwa na kisu  kilichofungwa katika karatasi nyeupe  kilichoandikwa kwa wino na kalamu ya blue maandishi yanayosomeka  kuwa LAZIMA  UFE  LEO.


Hata  hivyo  kando la mwili  wa kijana  huyo ambae alikuwa akipumua kwa mbali  kulikuwa na daftari  lililoandikwa kama kurasa 15 zenye  jumbe mbali mbali kwa wapenzi  wake ,ndugu na jamaa pamoja na Historia ya maisha  yake toka alipozaliwa hadi leo alipoamua  kukatisha maisha  yake.


Miongoni  mwa warembo  waliotajwa katika maandishi hayo ni pamoja na Nuru Mlowe  wa Ilembula ,Lucy  wa  Dar es Salaam ,Anna wa Moshi,Shangazi  Solina  wa Kilimanjaro ,James  Swale   wa Njombe ,Jack wa Tanga,mama Tunu  wa  Semtema,Elina wa Miyomboni ,MAGE wa  POSTA ,FARIDA  WA MBEYA na wengine  wengi pamoja na ujumbe  kwa mpenzi  wake  TUNU ambao  unasomeka  kuwa  TUNU SIAMINI KAMA  WEWE NDIO CHANZO  CHA  KIFO CHANGU KWANI MNENO MTAMU  ULIYOKUWA UNANPA TUKIWA TANGA?na mwisho  kila ujumbe  aliouandika aliweka  sahihi yake.


Kijana  huyo katika ujumbe  wake  wa maandishi  alisema kuwa ameamua  kujiua baada ya  kutoswa na pia tatizo la ugonjwa wa kansa na ugonjwa mwingine  unaomsumbua ambao hakuutaja katika maandishi yake.


Hata  hivyo tukio  hilo lilionyesha  kuwavuta  watu  wengi na baadhi yao kujiuliza TUPO WANGAPI? Kwani idadi ya  warembo  waliotajwa ilikuwa ni ndefu na si rahisi  kuimaliza kwa haraka huku  wakitaka vijana kuepuka  kuchukua uamuzi wa kujiua kwa kitu mapenzi.


Baadhi ya warembo  waliofika kushuhudia tukio  hilo walisema kuwa hata kama kijana huyo ametoswa na wapenzi wake  dawa haikuwa hiyo ya kujiua alipaswa  kutafuta  mwingine ama  wengine

 

Jitihada  za kuokoa maisha ya kijana  huyo zilizaa matanda baada ya  wasamaria wema pamoja na askari wa Doria  kufika eneo hilo na kumkimbiza kijana  huyo katika Hospitali ya mkoa ambako alipewa  maji ya Dripu mbili na kuyanywa na kabla ya  kupata nafuu na kutaja  jina lake na kuwa  yeye ni mkazi  wa Dar es Salaam aliyefika Njombe  kufuata mpenzi  wake aliyemaliza kidato cha nne na kuelezwa  kuwa  yupo Iringa na baada ya kumfuata mrembo huyo alianza kumzingua na yeye kuchukua uamuzi  huo.


Hata hivyo alidai kwa upande  wake alikula keki  yenye  sumu na sio alikunywa  sumu  hiyo japo alipoulizwa kuhusu ujumbe  wa maandishi alioacha katika daftari  hilo na mwingine  kujichora mkononi alisema kuwa alifanya  hivyo kama njia ya 
 kujiandaa kwa  kifo.

“Ndugu  zangu  mimi mwenzenu  ninatatizo la kupoteza fahamu kila ninapomkumbuka mpenzi  wangu  hivyo si mara ya  kwanza  kuanguka ni mara nyingi nikimuwazo Tunu huwa nazimia “


Hadi  tunakwenda mitamboni  mida ya saa 5 usiku kijana  huyo alikuwa katika chumba cha Daktari  wa Hospitali ya mkoa  wa Iringa  huku nje ulinzi  wa polisi  ukiwa  umetanda  kwa ajili ya kumchukulia hatua  zaidi ya  kutaka kujiua .
 Wananchi na askari  wakimpakia  kijana Kevin katika gari kumkimbiza Hospital ya mkoa wa Iringa .

No comments:

Post a Comment