Thursday, February 28, 2013

MTOTO WA MWENYEKITI WA KIJIJI TANANGOZI IRINGA AJINYONGA KATIKA OFISI YA KIJIJI



Katika hali ya kusikitisha  mtoto wa  mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Tanangozi katika wilaya ya  Iringa vijijini  Doto Kikoti ameamua kujinyonga katika ofisi ya kijiji  hicho inayoongozwa na babake mzazi kama njia ya kupinga kuwekwa kizuizini katika ofisi hiyo.

Tukio hilo  limetokea  usiku  wa kuamkia leo  baada ya kijana  huyo kutuhumiwa  kufanya  vurugu kubwa  katika kijiji  hicho na mzazi  wake  kuamua kumkamata na kumfungia katika  ofisi hiyo ya  kijiji kwa usalama  wake.

Wakizungumza na mtandao huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com mashuhuda wa  tukio  hilo  wamesema kuwa kijana  huyo alijinyonga kwa kutumia suluali  yake  akiwa ndani ya ofisi  hiyo baada ya mwenyekiti  wa kijiji  hicho ambae ni babake mzazi  Bw Narbeti Kikoti kumfungia katika ofisi hiyo.

Mwili  wa  kijana huyo umetolewa eneo la  ofisi hiyo majira ya saa 5 asubuhi  leo na kupelekwa nyumbani kwa  wazazi kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

No comments:

Post a Comment