Baba wa watoto hao Kanakulya akiwa na mmoja wa watoto zake aliyeokolewa katika janga hilo.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug)
Mtoto asiye na hatia amefariki dunia baada ya mama yake wa kambo kumfungia ndani ya nyumba pamoja na ndugu zake watatu wakiwa wamelala kisha akachoma nyumba moto.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku katika kijiji cha Namuyenje kilichopo katika wilaya ya Mukono.
Mtoto huyo Shafik Jjuuko mwenye umri wa miaka 6 alifariki kwa kukosa hewa wakati mama yake wa kambo Margaret Nampiima mwenye umri wa miaka 27 alipochoma moto nyumba waliokuwemo watoto hao huku baba yao ambaye ni dereva akiwa safarini.
Watoto wengine Sulaiman Mutebi 8, Shamim Nakimera, 9 na Hassan Geserwa ,11 waliokolewa wakiwa na majeraha yaliyosababishwa na moto huo ambao pia umeteketeza mali kadhaa.
Mtoto Ombeni Mbeula akiwa na mama yake Kilaudia Kigaila wakiwa hospitali kama umeguswa na hali ya mtoto huyu tafadhari tuma choche kwa njia ya M-Pesa 0757 498336 ili apata matibabu. (PICHA KWA HISANI YA PAMOJAPURE BLOG)
DODOMA, Tanzania
Nyumba
iliungua wakati watoto hao wamekaa ndani na wakati huo huo mama wa
mtoto alikuwa amekwenda shambani maeneo ya Chitemo iliyoko wilaya ya
mpwapwa.
Wakati
mvua inanyesha ghafla nyumba ilibomoka na wakati huohuo walikuwa watoto
wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo nyumba.
Baada ya tukio hilo
kutokea ikafanyika uokoaji kwenye nyumba hiyo maeneo ya Chitemo na
kufanikisha kuokoa watoto wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa
kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na huyu Ombeni Mbeula aliangukia
kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye picha lakin hali zao ni
salama kwa wote.
Baada
ya uokoaji waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospitali ya Mima
iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari wakamuagiza aende hospitali ya
Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili katika hospitali ya
mpwapwa na siku ya tatu wakaambiwa waende hospitali ya rufaa iliyoko
Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu zaidi.
Walipofika
katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakaanza matibabu lakini uwezo wa
kipato cha wazazi wake sio kizuri inahitajika msaada kwa matibabu maana
hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya matibabu haikuweza kupatikana
paka sasa
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio utajiri muokoe mtoto huyu maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa mbali sana.
Mama yake hana simu lakini anatumia simu ya ndugu yake Ekiria Paskali
Kwa yeyote atakayependa kumchangia mtoto huyo atume chochote kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii 0757 498336
No comments:
Post a Comment