Tangu kuuawa kwa kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda Osama bin Laden
kumekuwa na fununu nyingi zinazoeleeza mazingira ya kifo chake pamoja na
ujumla wa maisha yake wakati akiwa mafichoni. Katika mfulilizo wa
makala haya, Mwandishi George Njogopa amepitia simulizi za askari
aliyemuua kiongozi huyo kama alivyozungumza na mwandishi mmoja wa habari
nchini Marekani.
Akiwa mtu mwenye tabasamu na ucheshi wa mbali,
askari (jina linahifadhiwa) anatoa maelekezo kwa mwandishi wa habari
aliyetaka kujua historia ya maisha yake jeshini. Ndani ya mgahawa
uliofurika watu waliochangamka kwa vinywaji, askari mwanamaji anaanza
kueleza namna alivyojiunga na Jeshi la Wanamaji la Marekani hadi kufikia
nafasi ya kuwa mlenga shahaba mkuu.
Anasema anakumbuka kile kilichomsukuma kuchukua
uamuzi wa kujiunga na jeshi ni kama sehemu ya hasira iliyomkumba baada
ya kuachwa na mpenzi wake al iyedumu naye kwa kipindi kirefu.
“Unajua tukio la kuachwa na mpenzi wangu lilinivunja moyo sana… na ndiyo nikachukua uamuzi kwenda jeshini.
Anasema kuwa siku yake ya kwanza alipokwenda
kuomba kazi anakumbuka alimwambia ofisa mmoja wa jeshi kuwa alikuja hapo
kuomba kazi ya kulenga shahaba (sniper).
“Pale nilimkuta askari mfukuzi, mkufunzi
akaniuliza unataka nini… nikamwambia nataka kuwa mlenga shahaha, lakini
yeye akaniambia kuwa tayari walikuwa na walenga shabaha.
Hata hivyo alifaulu kuandikishwa na baadaye
kupelekwa kwenye mafunzo yaliyimwongezea ujuzi wa kazi na hatimaye
kuungana na vikosi vya wanajeshi wa maji vilivyosafiri sehemu mbalimbali
duniani. Kama ilivyo kwa askari wengi wanamaji, askari huyu alishiriki
kwenye operesheni mbalimbali za kijeshi ikiwemo zile zilizohusu katika
nchi za Afghanistan na Iraq.
Anasema operesheni yake kubwa ya kijeshi ilikuwa
nchini Afghanistan ambako vikosi vya Marekani vilivamia katika eneo hilo
katika kile kilichoelezwa na kukabiliana na utawala wa Taliban ambao
ulitajwa kuwa na ushirikiano wa karibu na Kundi la Kigaidi la Al-Qaeda.
“Uzoefu mkubwa wa kijeshi niliupata wakati nikiwa
Afghanistan ambako nakumbuka nilishiriki kikamilifu kukabiliana na
wanamgambo wa Taliban. Tulipofaulu kuwafurusha wanamgambo hao
tuliendelea kubakia nchini huko kuimarisha hali ya usalama na kusaidiana
na wananchi wa eneo lile kurejesha hali ya usalama.
“Kichwa changu kilikuwa tayari kimeshazoea mizinga
na makombora, maana wakati mwingine umekaa sehemu ghafla unasikia
kombora linavurumishwa mbele yako… Ghala nyuma unasikia mlio wa
bunduki.. Kusema kweli nilijifunza mengi wakati nikiwa Afganistan.
Wakati huo Marekani ilianzisha operesheni za
kukabiliana na Kundi la Al-Qaeda ambalo lililodaiwa kutekeleza tukio la
kigaida katika majengo yake mjini New York na Washington.
Shabaha ya Marekani ilikuwa kukabiliana na
kiongozi wa kundi hilo, Osama bin Laden ambaye wakati huo ilisemekana
amejichimbia mafichoni katika Milima ya Afghanistan.
No comments:
Post a Comment