Monday, February 11, 2013

CHADEMA WAPOTEZANA TENA NJOMBE :ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI AREJESHEWA UANACHAMA WAKE BAADA YA KUFUKUZWA.

 Ofisi za CHADEMA WILAYA YA nJOMBE ulikofanyika mkutano wa baraza la mashauriano la Wilaya.
 Aliyesimama ni katibu wa CHADEMA Jimbo la Njombe Magharibi bwana Abuu Mtamike akizungumza wakati wa Mkutano wa baraza la mashauriano la Wilaya ya Njombe.

 Huyu ni Kaimu katibu wa CHADEMA Wilaya ya Njombe akizungumza kwa msisitizo juu ya utovu wa baadhi ya viongozi wa Chama hicho.
 Aliyesimama ni mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Njombe Magharibi bwana Godlove Mdoe akizungumza wakati wa mkutano uliomrejeshea uanachama bwana Mathias Mwajombe.
Aliyekuwa katibu wa CHADEMA Wilaya ya Njombe bwana Chapwila aliyefukuzwa kwa tuhuma mbalimbali naye ahudhuria mkutano huo.
Kushoto ni ndugu Mathias Mwajombe aliyekuwa katibu wa CHADEMA Jimbo la Njombe Kaskazini akiwa kwenye mkutano uliomrejeshea uanachama wake baada ya kufukuzwa kwa utovu wa Nidhamu.

Baraza la Mashauriano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaani Njombe Limemrejesha Uwanachama wa Chama Hicho Aliyekuwa Katibu Chadema Jimbo la Njombe Kaskazini Bwana Mathias Mwajombe

Kurejeshwa Kwa Bwana Mwajombe Kumefuatia Agizo  Kutoka Makao Makuu ya Chadema Lililowataka Kumaliza Tofauti Hizo Kwa Ngazi ya Wilaya Pamoja na Barua Aliyoandika Mwanachama Huyo ya Kuomba Radhi na Kukiri Baadhi ya Makosa Aliyoyafanya.

Akitangaza Hatua Mwenyekiti wa  Kikao Hicho Ambaye Pia ni Mwenyekiti wa Jimbo la Njombe Magharaibi Bwana Godlove Mdoe Amesema Baraza Limemrejesha Bwana Mwajombe Kwa Masharti ya Kuwa Katika Matazamio ya Miezi Sita na Kutofanya Kazi za Chama Kama Kiongozi.
 
Bwana Mdoe Amesema Miongoni Mwa Mambo Yaliyopelekea Bwana Mwajombe Kufukuzwa Uongozi na Uanachama Wake ni Pamoja na Kukiuka Katiba ya Chama , Kutoa Siri za Chama na Kukaidi Agizo la Chama la Kutoa Majibu Katika Kipindi cha Mwezi Mmoja Kuhusiana na Tuhuma Zilizokuwa Zikimkabili.

Akizungumza Mara Baada ya Kureshwa Kuwa Mwanachama Bwana Mwajombe Amewashukuru Wajumbe wa Baraza Hilo Kwa Uamuzi Waliouchukuwa na Kuahidi Kuendelea Kupigania Haki na Kueneza Sera za Chama Hicho Kwa Nguvu Zake  Pamoja na Kushirikiana na Viongozi wa Chadema Kwa Ngazi Zote Ili Kuhakikisha Wanafikia Malengo ya Chama Hicho.

Mkutano Huo wa Baraza la Mashauriano la Chadema  Umefanyika Februari Tisa Mwaka Huu Kwenye Ofisi za Wilaya za Chama Hicho.
 

No comments:

Post a Comment