WATUMIAJI wa simu za mkononi nchini sasa watalazimika kuumia zaidi
kufuatia hatua ya Bunge kupendekeza kuanzishwa kodi mpya ya kadi za simu
za mkononi (Sim-Card), inayolenga kukusanya kiasi cha sh bilioni 255. 5
kwa mwaka.
Wakati Watanzania wakisubiri maumivu hayo, serikali imetumia kiasi cha
sh trilioni 1.8 kugharimia magari yake ya kifahari, maarufu kama
‘mashangingi’ kwa miaka mitatu tu, ikiwa ni zaidi ya bajeti ya Wizara ya
Afya kwa mwaka 2012/13 iliyotengewa sh trilioni 1.2.
Akisoma ripoti ya kamati maalumu iliyokabidhiwa kwa Spika Makinda jana,
Mwenyekiti wake, Andrew Chenge, alisema wameainisha maeneo 24 ambayo
kama yatafanyiwa kazi, yataliingizia taifa zaidi ya sh trilioni 3.9 kwa
mwaka wa fedha 2012/2013.
Eneo lingine lililoanishwa na kamati hiyo ni pamoja na kuanzisha kodi
mpya katika huduma za usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi
ambapo itaiingizia serikali kiasi cha sh bilioni 25.5.
No comments:
Post a Comment