MWANDISHI wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten
Tanga, Linus Kamafa amejeruhiwa vibaya na vijana waliokuwa wakichoma
matairi na kulipua baruti wakati wakisherehekea mkesha wa Mwaka Mpya.
Vijana hao wanadaiwa kumshambulia kwa mawe na
mapanga mwandishi huyo wa habari wakidhani ni miongoni mwa askari
Polisi waliokuwa wakipita mitaani kuzuia uchomaji moto wa matairi na
kulipua baruti.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na
kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe
ni kuwa mwandishi huyo wa habari alishambuliwa juzi saa 6.30 usiku
katika Mtaa wa Mapinduzi jijini hapa wakati akipiga picha za matukio ya
uchomaji wa matairi,baruti na kurusha mawe kwenye nyumba za watu.
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa
mwandishi huyo wa habari alijitokeza kwenye Mtaa wa Mapinduzi muda mfupi
mara baada ya gari la polisi kupita eneo hilo kwa lengo la kuzuia
uchomaji wa moto na wakaanza kumshambulia wakimtuhumu kuwa ni askari
aliyewapiga picha.
Akizungumza na Mwananchi Kamafa alisema, walianza
kumshambulia kwa mawe huku wakitaka kumnyang’anya kamera ndipo akaamua
kukimbia lakini alizingirwa na kushambuliwa hadi akaanguka chini na
kujeruhiwa magotini,mgongoni na kichwani. Alisema aliokolewa na watoto
wake waliomfuata baada ya kusikia akishambuliwa ndipo wakamkimbiza kituo
cha polisi cha Mabawa kwa ajili ya kupewa PF 3 na baadaye alifikishwa
hospitalini kupata matibabu.
Mwandishi huyo wa habari alisema katika kipindi cha nyuma cha mkesha wa Mwaka Mpya , vijana
No comments:
Post a Comment