Monday, November 12, 2012

waziri Malawi ajiuzulu ni mtoto wa aliyekuwa rais Mluzi



Austine Atupele Muluzi amejiuzulu uwaziri katika serikali ya Rais Joyce Banda wa nchi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia yake ya kugombea katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo.

Atupele Muluzi alikuwa akihudumu kama Waziri wa Mipango ya Uchumi na Maendeleo wa Malawi kama sehemu ya jitihada za bi. Banda za kugawa madaraka kati ya vyama mbalimbali vya nchi hiyo. Mwana huyo wa Bakili Muluzi anakusudia kugombea uraia kwa tiketi ya chama cha UDF katika uchaguzi ujao wa rais wa mwaka 2014, chama ambacho kiliwahi kutawala Malawi chini ya uongozi wa baba yake.

Atupele ametangaza hatua hiyo baada ya wafuasi wa chama tawala kinachoongozwa na Banda cha People’s Party (PP) kutoa matamshi mabaya kuhusu Bakili Muluzi na kuwataka watu kutomchagua mtu ambaye hajui lugha ya Kiyao na kwamba hana hadhi ya kuwa rais wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment