KATIBU WA chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa IPC bwana Frank Leonard akitoa mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari wa kituo cha Radio Uplands fm.
Wanahabari wa kituo cha UPLANDS FM RADIO NJOMBE WAKIWA KATIKA MAFUNZO
Waandishi wa Habari Wametakiwa Kuandika Habari ya Uchunguzi Zaidi Ili
Kuweza Kuibua Masuala Yaliyojificha na Yaliyosahaulika Ili Kuleta
Maendeleo Kwa Jamii na Kuacha Kuandika Habari za Warsha na Makongamano
Kwa Kiasi Kikubwa .
Rai Hiyo Imetolewa na Bwana Frank Leonard Wakati Akitoa Mafunzo
Siku Mbili Kwa Waandishi wa Habari wa Kituo cha Uplands Radio , na
Kusema Kuwa Waandishi Wengi wa Habari Huandika Habari za Vikao na Semina
Badala ya Kuandika Habari Zinazoigusa na Kusaidia Kutatua Changamoto
Zinazoikabili Jamii .
Katika Hatua Nyingine Mwezeshaji Huyo Amewataka Wanahabari Kuandika
Habari kwa Kuzingatia Maadili ya Kazi Yao Ili Kuepusha Madhara ya
Yanayoweza Kujitokeza Katika Jamii Ikiwemo Migogoro Katika Nchi na
Kufanya Kazi Kulingana na Misingi ya Uandishi wa Habari.
Kwa Upande Wao Washiriki wa Mafunzo Hayo Wamesema Yatawasaidia Katika
Utekelezaji wa Majukumu Yao ya Kila Siku na Kuongeza Kuwa Mafunzo Hayo
Yamewatoa Kutokana na Kufanyakazi Kwa Kutumia Mfumo wa Zamani wa
Uandishi Habari.
No comments:
Post a Comment