MWANAMKE mmoja wa eneo la Majengo, jijini Mbeya, anadaiwa
kummwagia maji ya moto, kumfungia ndani na hatimaye, kumlazimisha kula
kinyesi, mtoto wa dada yake.
Akizungumza katika eneo la tukio, Mwenyekiti wa
Mtaa wa Majengo, Habiba Mwakitabu, alisema tukio hilo lilitokea juzi
na kwamba liligunduliwa na majirani wa mwanamke huyo, baada ya kusikia
sauti ya mtoto huyo akilia kwa maumivu.
Alisema baada ya kusikia kilio hicho, majirani hao walikwenda katika eneo hilo na kiini cha mtoto huyo kuteswa.
Mwakitabu alisema hata hivyo, mwanamke huyo
alishindwa kutoa ushirikiano, jambo lililowalazimisha wananchi kuanza
kumshambulia kwa kipigo .
Mwenyekiti huyo alisema baadaye, majirani
walibomoa mlango wa nyumba na walipoingia ndani, walimkuta mtoto huyo
akiwa uchi huku sehemu mbalimbali za mwili wake, zikiwa zinmeungua
vibaya.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa mtaa, upande mkono wa kushoto wa mwili wa mtoto huyo, ndiyo uliokuwa umeathirika zaidi.
Mwakitabu alisema katika mahojiano naye, mtoto
huyo, alidai kuwa majeraha hayo yalitokana na mama yake mdogo kumfunga
mikononi na kisha kumwagia maji ya moto na baadaye, kumlazimisha kula
kinyesi chake hali.
Kwa mujibu wa mwenyekiti, maelezo hayo yaliwafanya wananchi kupandwa na jazba kiasi cha kuta kumshambulia tena mama huyo.
Habari za awali zilisema, mtuhumiwa amekuwa
akimfanya mtoto huyo ukatili wa mara kwa mara, licha ya jitihada za
kumtaka aache kufanya hivyo.
Diwani wa Kata ya Majengo, Samuel Mamboma,
aliwasili katika eneo hilo na kumbnusuru mama huyo kwa kumpeleka polisi
akiwa na mtoto huyo ambaye baadaye alipelekwa hospitalini kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment