Waandamanaji wapinga mkutano wa Viongozi wa G7
Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel, kushoto, na Rais wa Marekani Barack Obama
wanakaribishwa na weakazi wa kijiji cha Kruen, kusini mwa Ujerumani June
7, 2015.
Viongozi wa mataifa saba tajri duniani wanakutana Ujerumani
Jumapili, katika mji wa mapumziko wa Garmisch Partenkirchen, kwa mkutano
wa kila mwaka wa siku mbili, kujadili mizozo mbali mbali ya kimataifa,
pamoja na masuala ya uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa, na vita dhidi
ya ISIS.
Rais Barack Obama akifuatana na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel
walitembelea kijiji kimoja karibu na eneo la mkutano Jumapili asubuhi,
na kusema kwamba mnamo siku mbili watajadili kile alichokieleza ni
"changamoto ngumu", zinazokabili dunia.
Amesema, "tutajadili mustakbal wetu wa pamoja, uchumi wa kimataifa
ambao utabuni nafasi za ajira, kuhakikisha Umoja wa Ulaya unaendelea
kuwa na nguvu na ufanisi, kubuni ushirika mpya wa biashara kati ya
mataifa ya Ulaya na Amerika, na kukabiliana na uvamizi wa Rashia huko
Ukraine, pamoja na kupambana na kitisho kutokana na mabadiliko makubwa
ya hali ya hewa."
Viongozi hao wanatarajiwa kukubaliana juu ya kuendelea na vikwazo
dhidi ya rashia, ambayo ilikuwa mwanachama wa kundi hilo hadi pale
ilipoivamia na kukalia jimbo la Crimea, mashariki ya Ukriane mwaka jana.
No comments:
Post a Comment