Rais wa Uturuki, Recep Tayyip
Erdogan, ametoa wito kwa vyama vyote vya kisiasa Nchini humo, kufanya
kazi pamoja na kuhakikisha kuwa kuna mazingira mazuri ya kujiamini na
kuleta utulivu kote Nchini humo.
Hotuba yake inakuja baada ya
matokeo ya ubunge kutangazwa hapo jana Jumapili ambapo chama chake
kilipata pigo kubwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka kumi na
mitatu iliyopita.
Hakuna chama ambacho kimekubali kuunda serikali ya muungano.
Mwaandishi
wa BBC Nchini Uturuki amesema kuwa chama cha AK huenda kikajaribu
kuunda serikali ya wachache Bungeni, jambao ambalo si dhabiti.
Iwapo
hakutakuwa na serikali itakayoundwa kwa kipindi ha siku arobaini na
tano zinazokuja, hakutakuwa na jingine ila kuitishwa kwa uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment