Alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis alifahamika kwa kutoroka usiku na kuwatafuta watu, kuzungumza nao na wakati mwingine kuwanunulia chakula.PICHA MAKTABA
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.
Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao
usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu
Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedha toka
kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.
Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa
akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada
maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.
Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa
Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda
kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.
“Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda
kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda
kufanya kazi hiyo,” alisema Padri Krajewski.
Hata hivyo, alipoulizwa iwapo Papa aliwahi kwenda naye nje ya mji kwa ajili hiyo, Askofu Krajewski, alisita kujibu swali hilo.
Wakati huohuo, gazeti la Huffington Post
limeripoti kuwa walinzi wa Uswisi, wamethibitisha kuwa Papa amekuwa
akizunguka maeneo mbalimbali usiku akiwa amevalia mavazi ya kawaida ya
wachungaji na kuwapa misaada, wanaume na wanawake wenye shida
mbalimbali.
Tangu kuteuliwa kwake, papa Francis amevipamba
vichwa vya habari duniani baada ya kuonekana akijaribu kuvaa kofia za
polisi wa zimamoto, kuwaruhusu vijana wadogo wa kiume kuibusu miguu yake
na kuwapigia simu waumini wake na kuzungumza nao.
Hivi karibuni, aliripotiwa katika vyombo vya
habari akiwabusu na kuwafariji waumini walemavu katika Kanisa la
Mtakatifu Peter, huku taarifa nyingine zikionyesha kuwa ametuma fedha
zake binafsi kwa wahamiaji na wanaohangaikia mafao yao.
Alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires,
Papa Francis alifahamika kwa kutoroka usiku na kuwatafuta watu,
kuzungumza nao na wakati mwingine kuwanunulia chakula.
Mapapa wengine waliopita pia wametajwa kutoroka
usiku, kwa mfano papa John wa X111 alikuwa na tabia ya kutoroka usiku na
kwenda mitaa ya Rome kufurahia uzuri wa jiji hilo, wakati Papa Pius wa
X11alivalia kama Mfaransa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kwenda
mipakani kuwasaidia Wayahudi wa Kirumi kisha kuwaweka katika sehemu
salama.
No comments:
Post a Comment