Mzee Nelson “Madiba” Mandela amefariki dunia kwa mujibu wa CNN mzee
Madiba amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 95.Kwa mujibu wa Rais
wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema mzee Mandela amefariki
Ijumaa usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu.Anatarajiwa kuzikwa baada ya
siku 10 zijazo.
RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini na mpinga siasa za ubaguzi wa
rangi, Nelson Mandela amefariki nchini humo akiwa na umri wa miaka 95.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais wa nchi
hiyo, Jacob Zuma ambaye amesema Mandela amefariki majira ya saa 2.50
usiku wa Alhamisi kwa saa za Afrika Kusini.
Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye
mapafu kwa muda mrefu, alilazwa na baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali
ambapo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.
Tayari viongozi mbalimbali duaniani wameshaanza kutuma salamu za rambirambi kwa familia na taifa la Afrika Kusini.
Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon.
No comments:
Post a Comment