Wednesday, December 4, 2013

BOMU LAOKOTWA SHAMBANI

 
Bomu limeokotwa karibu na eneo la Kanisa la Huduma ya Maombezi ambalo pia
ni eneo la makazi ya watu katika barabara ya Barakuda Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro.
Bomu hilo liliokotwa juzi  asubuhi na mtoto ambaye alikuwa akilima bustani jirani na nyumba yao  na baada kuchimbua udongo aliona kitu kizito na kukitoa.

Mmoja mashuuda, Brayton Sospeter, alisema bomu hilo liliokotwa na mtoto huyo na baadaye kulichukua na kwenda kuwaonyesha watoto wenzake waliokuwa wakicheza katika eneo hilo.

Alisema watoto hao waliendelea kulichezea na baadaye kumuonyesha mzee mmoja liyekuwa akipita katika eneo hilo na kugundua kuwa ni bomu, hivyo kutoa taarifa Polisi.

Sospeter alisema baadaye  Polisi walifika katika eneo hilo na kuthibitisha kuwa ni bomu na kueleza kuwa ni kubwa hivyo hawana uwezo wa kulitoa katika eneo hilo na badala yake walizungushia uzio huku wakiahidi kwenda kuwasilina na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kulitoa katika eneo hilo.Hata hivyo wanajeshi hawakufika.

Naye mmoja wa waumini wa kanisa hilo, alijitambulisha kwa jina la mama Maloda, alilalamikia vyombo vya usalama kutoliondoa licya ya kuthibitisha kuwa ni bomu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, John Laswai, alithibitisha kuwepo kwa taarifa hizo na kwamba walikuwa wakiwasilina na JWTZ ili kwenda kulitambua.
Hadi jana mchana, bomu hilo liliendelea kuwapo eneo hilo bila JWTZ kufika.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment