Taasisi isiyo ya kiserikali
inayoshughulikia mambo ya utawala bora na maendeleo nchini (The Center
for Good Governance and Development in Tanzania -CEGODETA), imeitaka
Serikali ya Tanzania kumshtaki Rais wa Malawi, Joyce Banda Umoja wa Nchi
za Afrika (AU).
Taarifa ya taasisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya ilisema uamuzi huo ni
kutokana na kauli za dharau za Banda dhidi ya viongozi wanaoshughulikia
mgogoro wa Ziwa Nyasa.
“Serikali imshtaki kiongozi huyo wa Malawi AU ili
aulizwe ana dhamira gani kwa Tanzania na Afrika kabla hajaleta madhara
makubwa kwa nchi yetu na Bara zima la Afrika.
Waswahili husema ‘Mchelea mwana kulia hulia yeye’
na ‘Mdharau mwiba mguu huota tende’, maana yake ni kuwa inawezekana huyu
mtu ana mtandao mbaya sana tusioujua, tufanye uchunguzi kuubaini,”
inasema taarifa hiyo.
Inasema kuwa, mara tu baada ya kuingia madarakani
Rais Banda alidai kuwa Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa asilimia 100 na
Tanzania haina haki ya kulitumia ziwa hilo kwa njia yoyote ile.
Taarifa hiyo inasema kuwa, mgogoro huo kwa sasa
uko kwenye jopo la usuluhishi la marais wastaafu wa nchi za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) chini ya Rais Mstaafu, Joachim
Chissano wa Msumbiji.
No comments:
Post a Comment