Wednesday, November 27, 2013

MAN UNITED WANUSURIKA KUPATA AJALI YA NDEGE WAKIELEKEA UJERUMANI KUCHEZA NA BAYER LEVERKUSEN


 


Manchester United jana nusura wapate ajali kama iliyowahi kuwakumba miaka kadhaa iliyopita huko Munich baada ya ndege waliyopanda kusitisha zoezi la kutua mita 400 kutoka kwenye sehemu ya kutulia ndege kwenye uwanja wa Konrad Adenauer uliopo huko Cologne Ujerumani.
Ndege ya shirika la Monarch Airlines A321, namba MON 9254, ilipangwa kutua uwanjani hapo  5.30pm kwa muda wa Ujerumani, lakini rubani alilazimika kusitisha kutua kwa ndege hiyo kwa sababu kulikuwa na ndege nyingine kwenye sehemu ya kutulia. Ndege hiyo waliyopanda United ikabidi izunguke uwanja hewani na kuja kutua dakika 10 baadae saa 5.40pm.
Abiria mmoja katika ndege hiyo, ambayo ilikuwa na wachezaji wote wa United na maofisa wengine wa timu hiyo akiwemo CEO wa zamani wa klabu hiyo David Gill waliokuwa wakielekea kwenye mchezo wa klabu bingwa ya ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen, alisema kwamba tukio hilo lileta hali ya kutisha miongoni mwa abiria huku akifhamika kwamba ilitolewa taarifa rasmi kwamba kulikuwa na tatizo lilokuwa likiendelea. 
Mlinzi wa United Rio Ferdinand alitweet kuhusu tukio hilo muda mfupi baada ya kutua salama akisema, 'Landed in Germany....just....I’ve only just recovered after that choppy landing!
Kwenye msafara huo hakuwemo Sir Bobby Charlton, mtu mmojawapo aliyenusurika katika ajali iliyopita ya Munich, pia hakuwemo kocha mstaafu wa timu hiyo Sir Alex Ferguson.
Pamoja na kuchelewa kutua kwa ndege hiyo huko Cologne, Moyes na mlinzi Chris Smalling walienda kwenye mkutano wa waandishi wa habari wakiwa watulivu na wasiokuwa na chembe ya wasiwasi juu ya tukio hilo. 
Usiku wa leo United inacheza mechi muhimu na Leverkusen huku wakiwa wana mapengo ya wachezaji wao muhimu kama Van Persie, Carrick, Jones na Vidic.

RATIBA YA MECHI NYINGINE ZA LEO




MATOKEO YA JANA
Group E
Basel 1-0 Chelsea
Steaua Bucuresti 0-0 Schalke 04

Group F
Arsenal 2-0 Marseille
Borussia Dortmund 3-1 Napoli

Group G
Zenit Petersburg 1-1 Atletico Madrid
FC Porto 1-1 Austria Wien

Group H
Ajax 2-1 Barcelona
Celtic 0-3 AC Milan


No comments:

Post a Comment