Watu wawili wamefariki dunia
akiwemo mtoto mwenye umri wa siku moja ambaye maiti yake imekutwa
kwenye nyumba ambayo haijakamilika ujenzi (pagale), katika matukio
yaliyoripotiwa juzi jijini Dar es Salaam.
Katika tukio la pili, mwanamume mmoja amefariki
dunia baada ya kuanguka wakati akijaribu kuangua nazi kwa kutumia fimbo
na kusababisha kichwa chake kupasuka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi
alisema katika tukio la kwanza, maiti ya mtoto wa kike mwenye umri wa
siku moja iliokotwa kwenye nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake.
Minagi alisema tukio hilo lilitokea Novemba 24,
mwaka huu ambapo maiti hiyo ilikutwa imetupwa katika nyumba hiyo, huku
ikiwa haina jeraha. Hata hivyo hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio
hilo na polisi wanaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo na maiti
yamehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika tukio la pili, Mkazi wa Mjimwema Songambele
Shija (60) amekutwa amekufa huku kichwa chake kikiwa kimepasuliwa na
matofali yaliyodondoka kutoka kwenye nyumba ambayo haijakamilika ujenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engilbert Kiondo
alisema tukio hilo limetokea Novemba 21 mwaka huu saa 7:00 mchana
katika eneo la Ungindoni Jangwani Wilaya ya Temeke. Kiondo alisema
chanzo cha kifo chake inasadikiwa kuwa marehemu enzi za uhai wake
alipanda juu ya pagala hilo kwa kutumia stuli ili aweze kuangua nazi
kwenye mnazi uliopo karibu na nyumba hiyo.
Alisema alitumia fimbo ndefu yenye ndoano
kuangulia nazi hizo huku akiwa amepanda juu ya ukuta huo ambapo
ulishindwa kuhimili uzito huo na kuporomoka na kusababisha kifo chake.
No comments:
Post a Comment