Naibu Waziri wa Maji, Dk.
Binilith Mahenge ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji
mkoani Singida.
Dk. Mahenge amesema hayo
akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida kukagua miradi ya maji katika
Halmashauri za Wilaya ya mkoa huo.
Dk. Mahenge alifurahia
utendaji kazi wa mkandarasi wa mradi wa maji wa kijiji cha Ng’unguli, kwa hatua
iliyofikiwa licha ya kuwa na miezi mitatu tu tangu ianze na kuahidiwa kuwa
mpaka mwezi ujao utakuwa umekamilika. Huku akisisitiza viongozi waelekeze nguvu
katika miradi mingine itekelezwe kwa wakati na maji yapatikane.
Mkoa wa Singida umepokea Sh.
Bil 41.5 kwa robo ya kwanza ya mgao wa fedha mwaka 2013/14 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya vijiji 10 na programu ya BRN.
Dk. Mahenge amemaliza ziara
yake ya mikoa ya Dodoma
na Singida mwishoni mwa wiki, katika kuhakikisha utekelezaji wa awamu ya kwanza
ya programu ya wa Big Results Now na miradi yote ya maji inatekelezwa kwa kasi
na ufanisi ili kuleta matokeo yaliyopangwa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment