na Furahisha Nundu
MAKETE
Wanafunzi wa shule ya
sekondari Lupaliloiliyopo wilayani Makete wameelezea kupanda kwa kiwango cha
Taaluma kwa wanafunzi shuleni hapo
Wakizungumza na mtandao huu wamesema kuwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi
umeongezeka kutoka asilimia 65-kufikia 90 kulingana na jitihada za walimu
pamoja na kujisomea wanafunzi wenyewe pindi wanapokuwa shuleni na majumbani
Shule hiyo inayoongozwa na
M/kuu Liombo yenye zaidi ya wanafunzi 600 na walimu 25 na masomo yanayofundishwa
ni sayansi pamoja na sanaa ikiwa shule hiyo ina mazingira yenye mvuto kwa
kujisomea wanafunzi
Wakizungumzia suala la baadhi
ya wanafunzi wa kike kupata mimba wawapo shuleni wamesema kuwa baadhi ya shule
mazingira wa wanafunzi wa kike kuishi nje ya bweni ni moja ya sababu
zinazofanya mwanafunzi kupata mamba
Hata hivyo wamewataka
wanafunzi wengine nchini kujikinga na suala hilo na kupunguza utoro shuleni ili kuongeza
kiwango cha elimu wilayani hapa na nchi nzima
No comments:
Post a Comment