SERIKALI
imepandisha bei ya umeme kama Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
lilivyoomba hivi karibuni kutaka kuongeza gharama za nishati hiyo kwa
asilimia 68.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene, wakati alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha
Kumepambazuka kinachorushwa na kituo cha Redio One.
Alisema ni ukweli usiopingika kuwa hata TANESCO ikiongeza gharama za
umeme hadi kufikia sh 800 kwa uniti bado bei hiyo itaendelea kuwa nafuu
ukilinganisha na gharama za kununua mafuta ya taa.
Simbachawene alitoa tahadhari kwamba endapo kuna mwananchi yeyote
atakayeona gharama za umeme ni kubwa ni vema akaamua kuwasha kibatari au
akae giza.
Ni hivi karibuni shirika hilo liliomba kuongeza bei ya umeme kwa
asilimia 67.87 ikiwa ni kutoka sh 197.8 kwa Uniti mpaka sh 332.06.
No comments:
Post a Comment