BAADHI ya wananchi Wilayani Kyela Mkoani Mbeya wamezipongeza juhudi zinzofanywa na kanisa la maombezi la Temple of prayer all nations churh(TPFNC) kwa kazi kubwa inayoifanywa na wachungaji ya kuombea wagonjwa ambao wanapona baada ya kupokea uponyaji kutokana na maombezi yanayofanywa kanisani hapo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya maombezi hayo walitoa ushuhuda ambapo walidai kuwa wamepata tumaini jipya baada ya watu wanaougua magonjwa ya hajabu na wale wenyeshida mbalimbali kuondokana na shida hizo pindi wapatapo maombezi yanayoambatana na upakwaji wa mafuta ya uzima pindi waendapo kanisani hapo.
Dorris Crement mkazi wa kijiji cha Lupaso kata ya Kajunjumele alisema kuwa yeye alipata matatizo ya kuvumba mguu tangu mwanzoni mwa mwezi huu na alizunguka katika hospitali kadhaa na kwa waganga wa tiba mbadala kwa lengo la kupata tiba lakini hakufanikiwa kupona na kuwa alifika kanisani hapo baada ya kupewa taarifa na sasa amepona baada ya kufanyiwa maombi na kupakwa mafuta.
Vessy potes (13) kutoka kata ya Bujonde ambaye ni mwana funzi wa darasa la saba shule ya msingi Isanga alisema alianza kusumbuliwa na sikio tangu mwezi wa sita mwaka huu baada ya kutibiwa katika hospitali ya Wilaya homa ilizidi na ilipofika siku ya saba ya matibabu yake alipata tatizo lingine la kupooza na baada ya matibabu ya hospitalini kushindikana alipelekwa na wazazi wake katika kanisa hilo la maombezi na amepona mara baada ya kuombewa na kupakwa mafuta ya upako.
Dukra Ngatunga (13) mkazi wa Ilomba Mbeya na ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza Lyoto sekondari alisema kuwa yeye alifiwa na pacha wake mara baada ya kufa pacha huyo alimwita ili naye afe wakaishi wote katika sayari nyingine naye alijikuta akinywa sumu ya panya lakini hakuweza kufa baadaye alitafuta mabetri matatu ya redio na kuyasaga na kunywa baadaye alilegea lakini hakufa.
Mama mzazi wa mtoto huyo Nuru Mwakyeru alisema walipomuona mtoto huyo walimhoji ambaye naye aliwaeleza kuwa anaitwa na pacha wake aliyetangulia mbele za haki ili wakaishi wote katika sayari mpya ndipo walipomkimbiza hospitalini na madaktari walifanikiwa kumchoma sindano ya kuondoa sumu mwilini lakini waliporudi nyuimbani hali ilizidi kuwa mbaya.
Aliongeza kuwa baada ya hali hiyo kuzidi kuwa mbaya waliamua kusafiri hadi Wilayani Kyela kwa lengo la kupata huduma ya maombezi inayofanywa kanisani hapo na kuwa walipofika walipokelewa na watumishi wa kanisa hilo ambao walifanya maombi kwa dadika 15 na kumpaka mafuta ya upako ndipo hali ya mtoto wake ikaendelea kuimalika na siku iliyofuata akapona kabisa na kurejea nyumbani.
Mchungaji wa Kanisa hilo ambaye alijitenga na askofu wake Mullilege mkombo(mzee wa yesu)na kuanzisha kanisa lake Nabii Charles Mkuvasa alisema kuwa kanisa lake limekuwa kama hospitali ya rufaa kwa kuwa wagonjwa wengi na watu wenyeshida mbalimbali wanaokuja kwake wanapona pindi anapowaombea na wao kupokea uponjaji kutoka kwa yesu Kristo.
Mkuvasa aliongeza kuwa hivi sasa anakosa usingizi baada ya wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na wa Nchi jirani ya Malawi wanaofika kanisani hapo kwa wingi ambao amekuwa akiawafanyia maombi mfululizo usiku na mchana hivyo kukosa muda wa kupumzika na kwamba hivi sasa anatarajia kufungua matawi vijijini ili kurahisisha na kusogeza huduma kwa jamii na jamii hiyo inatakiwa kumshirikisha mungu kwa kila jambo ili kukwepa majaribu ya Ibilisi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment