Wednesday, August 7, 2013

MLUGO ACHAFUA JIMBO LA MWAKYEMBE

 waziri mullugo akiwahutubia wazazi na wanafunzi katika mahafari ya kwanza kwenye chuo cha KPC Wilayani kyela. na picha ya pili ni waziri  Mwakyembe akiwa na viongozi kadhaa waliohudhuria sherehe hizo za mahafari
IMEELEZWA kuwa mwamko mdogo wa kielimu kwa Wazazi wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya ndicho chanzo cha kupelekea wilaya hiyo kushika nafasi ya kwanza kufanya vibaya kimkoa katika nyanja ya elimu nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Phillipo Mulugo wakati wa mahafari ya kwanza ya Chuo cha Ufundi na Biashara Kyela (Kyela Polytechnic College) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.

Mh. Mulugo alisema kuwa wilaya ya Kyela ni miongoni mwa wilaya 40 ambazo zimekuwa zinafanya vibaya katika suala la elimu na kwamba ni wilaya ambayo inashika nafasi ya kwanza kimkoa.

Alisema kuwa kutokana na mwamko mdogo wa wazazi kielimu ndiyo maana chuo hicho kimekuwa na wanafunzi wachache tofauti na mikoa mingine ambayo imekuwa na vyuo vichache lakini wanafunzi ni wengi kutokana na wazizi kuhimiza watoto wao kujikita katika masomo.

“Ni heri niache ubunge wangu kuliko kuangalia suala baya kama hili  wilayani Kyela likiachwa kama ilivyo kwa kuwa hii ni aibu kwetu sote hasa wakazi wa Wilaya hii na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla” alisema Mulugo.

Aliongeza kuwa kutokana na tatizo hilo Serikali imeiingiza Wilaya hiyo kuwa miongoni mwa wilaya ambazo zimepewa kipaumbele katika utekelezaji wa  ‘Big result now’ yaani mambo makubwa sasa ili kuongeza ufanisi katika uchapaji kazi.

Waziri huyo alisema kutokana na uanzishwaji wa kauli mbiu hiyo na Rais nilazima viongozi wawajibike ipasavyo katika kusimamia suala hilo na kudai kuwa ikiwezekana walimu wakuu na maAfisa elimu wawajibishwe iwapo watathibitika kufanya uzembe katika jambo hili.

Aliongeza kuwa kunabaadhi ya waalimu Wilayani hapa wamekuwa na kawaida ya kunywa pombe hasubuhi nyakati za masomo na kufanya vibaya katika vipindi vyao pindi wanapo fundisha na kuwa amemuagiza mkuu wa Wilaya Magreti Malenga kuwashughurikia waalimu watakaobainika kufanya hivyo.

“Natoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anafuatilia ufundishaji wa walimu mashuleni kwani kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakinywa pombe majira ya asubuhi tena wakati wa kazi jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa watoto” aliongeza Mulugo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Salatiel Mwakyambiki alisema kuwa Kyela inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya Biashara ndogo ndogo na matumizi ya simu wawapo darasani ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike, na baadhi ya vijana wa kiume.

Aidha alitaja changamoto nyingine kuwa ni matumizi ya simu ambapo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakitumia mawasiliano wakiwa darasani jambo ambalo alisema kuwa limeongeza kupunguza nidhamu kwa wanafunzi.

Mbunge wa Jimbo hilo Dr,Harrison Mwakyembe kwa upande wake amewataka wazazi kuwahimiza watoto wao kujikita katika elimu katika kujiunga na vyuo ili kuondokana na haibu hii ya kuwa wa mwisho kimkoa katika sekta ya eli

No comments:

Post a Comment