Tuesday, July 30, 2013

Kairuki -Vyeti vya kuzaliwa usigeuzwe mradi kujipatia kipato


Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
 
SERIKALI nchini  imewataka wakurugenzi wote wa Halamashauri  ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa masuala  ya usajili wa vizazi na vifo  nchini kuhakikisha kuwa,usajili unafanyika kwa asilimia mia moja  kwenye halmashauri zao.
Kauli hiyo imetolewa juzi na Naibu waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki katika Mkutano wa uzinduzi wa  mpango  mpya wa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kutoka ofisi ya Mkuu wa wilayani, na kuwa chini ya Mkurugenzi wa Hamashari uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Ruanda Nzovwe jiji ni Mbeya.
Kairuki ambaye alkuwa mgeni Rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa ni vema wakuregenzi hao wakawa makini katika mfumo huo mpya,  ambao serikari imelenga kuwa punguzia usumbufu wananchi  kwani hivi sasa vyeti hivyo  vitakuwa vikitolewa katika ngzi ya kata huku maafisa watendaji wa kati wakipewa jukumu hilo.
Akiwahutumia mamaia ya wananchi  walio hudhuiria uzinduzi  huo ulioandaliwa na wakakala wa vizazi na vifo  RITA  Kairuki alisema kuwa  kwa mujibu wa sheria, usajili wa vizazi na vifo unafanyika kwa wale waliozalia Tanzania bara na kwamba ni wajibu kwa watewndaji wote wanao husika na usajili kuzingatia matakwa ya sheria.
Alisema kuwa Serikali uimechukkua jukumu vyeti hivyoo vtatolewa kwa watoto wenye kuanzia mwaka 0-5 ni burte na kwamba  vyeti hivyom  vitatolewa bure, na kuwa taka wananchi wasikubali kununua vyeti hivyo endepo patatokea watendaji wachache wasio waaminifu wanao taka kugeuza mradi zoezi hilo.
Mbali na wito huo Waziri Kairuki alisema kuwa ni vema wazazi wenye watoto chini ya umri wa miaka hiyo  wakajitokeza kwa wingi katika zoezi hilo kwani kujianadikisha na kujua idadi ya watu unakuwa msaada mkubwa kwa serikali  kuweza kutoa huduma katika maeneop husika kulingana na  idadi kamili katika maeneo husika hasa pale inapoi taka kutoa huduma za kijamii  katika elimu, afya na miundombinu.
Aidha Kairuki alizitaka ofisi za watendaji kata na serikali kufanya uahamsishaji  katika maeneo yao kupitia mikutano ya wananchi sambamba na kuweka utaratibu wa kufanya uahikiki wa kila baada miezi mitatu kama kila mototo katika eneo lake amesha pata huduma hiyo.
Aidha katika taarifa ya Rita Mwenekiti wa bodi ya RITA Vicent Mrisho katika taarifa yake kwa mgeni rasmi alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za nchi ni asilimia  14 tu ya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano wamesajiliwa na kati yao ni asalimia 7.7 ndiyo wenye vyeti vya kuzaliwa.
Alisema kutokana takwimu  hizo kutoridhisha na kwa kutambua umuhimu wa usajili wa kumbukumbu muhumu za Vizazi mwaka 2011 RITA kwa kushirikina na wadau wa mbalimbali ilibini mkakati wa usajili wa watoto wa umri wa chini ya miaka hiyo ulilenga kuboresha hali ya usajIli nchini na kuweka kipaumbele kwa watoito wenye chinya miaka mitano.
Katika  uzinduzi huo ambao ulihudhiwa pia na wakurugenzi kutoka JHalamashauri za Mkoa wa Mbeya na wakuu wa wilaya na wabunge wa jimbo la Mbeya ,na  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi  aliwataka wananchi kujihitokeza kwa wingi katika zoezi zima kwani maendeleo yeyote dunia yantegemea sana kujua idadi ya watu na kwamba suala hilo siyo la kisiasa bali ni la kimaendelo hivyo wanachi wa Mbeya na wilaya zingine hawana budi kuisapoti serikali katika kutekleza azma hiyo.
Uandikishwaji na utoaji wa vyeti vya kuazaliwa unatajiwa kuanza kutolewa Mkoani hapa Juni 25 katika wilaya  za Momba, Mbozi,Mbeya jiji na kwamba mara baada kamalizika itafuta mikoa ya Mwanza, Shimiwi,Shinyanga, na Getita na kwamba a mpango huo unafadhiliwa na serikali ya Tanzania kuishirikiana na shirika la watoto dunia Unicef,na kampuni ya simu za  Mkononi ya Tigo.
mwisho
 
 
 

No comments:

Post a Comment