Mwanafunzi U.D.S atoa
ushuhuda jinsi anavyo tumiwa kuzisafirisha
MUUNGANO Vijana wa
madhehebu ya kikristo Mkoani Mbeya,wametishia
kutangaza na kuweka hadharani
majina ya mapapa wanaojihusisha na biashara ya
madawa ya kulevya hapa nchini.
Tamko hilo limetolewa juzi na Muungano wa vijana wa kikristo wakati
kongamano la kuhubiri injili na kuliombea taifa mkoani Mbeya lililofanyika katika kanisa la Tanzania Assemblies of
God Calvary Temple lililopo eneo
la Uyole Jijini hapa sambamba kupinga na
kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana kwa kuwa ndiyo waathirika
wakubwa na madawa hayo.
Akizungumza na Tanzania daima katika viwanja vya kanisa hilo
Mchungaji Williamu Mwamalanga wa kanisa la
Pentekoste alisema kuwa vijana wa madhehebu hayo wameamua kufanya kongamano hilo ili kuishinikiza serikali ili kuchukua hatua dhidi ya wauza
madawa.
Alisema kuwa endapo serekali haita chukua hatua dhidi ya
vigogo wanao jihusisha na biashara hiyo haramu, vijina hao walisema wapo tayari
kuanika majina ya watu maarufu wanao fanya biashara hiyo ambayo ni hatari kwa
amani, utulivu na usalama wa nchi.
Mchungaji Mwamalanga alisema kuwa biashara ya madawa ya
kulevya ni uvunjifu wa haki, na nchi
imepoteza amani kwa kuwa dawa za kulevya zimewafavya vijana wengi wa kitanzania
kupoteza haki na uzalendo kwa taifa lao
‘Vijana wameamua kuliombea taifa ili kuwarudisha vijana
katika kumrudia mungu pia,vijana wamesema kuwa wanatoa siku saba kwa vigogo
kuacha tabia ya kuingiza dawa za kulevya hapa nchini ambapo limekuwa janga kwa
taifa’ Alisema Mchungaji Mwamalanga.
Mbali na kutaja majina ya mapapa wa madawa ya kulevya hapa
nchini walisema kuwa wapo tayari kuzitaja baadhi ya nchi ambazo zinaonyesha kushirika
katika biashara ya madawa ya kulevya na
kwamba balozi zote zitapatiwa majina ya vigogo hao.
Alisema serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kwa
mapapa hao ambao wamekuwa wanatumia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Nyerere
kama sehemu ya kupokea na kuyapitisha madawa
ya kulevya bila kudhibiti hali hiyo inapelekea serikali itapoteza heshima
kimataifa.
Katika kongamano hilo lililo kuwa na kauli mbiu ya “haki inalinua
taifa” mwanafunzi wa chuo kikuu cha
Dar-es-salaamu mwaka wa tatu alitoa ushuhuda wa jinsi alivyo
kuwa akitumiwa na baadhi ya wafanyabiasha hapa nchini kusafirisha dawa hizo,sambamba na hilo
mwanafunzi (jina tunalo) aliamua kusalimisha
Kg (5) tano za madawa ya kulevywa
aina ya Heroine ambazo alikuwa ameingia nazo Mkoa Mbeya kutoka Jijini Dar-es-salaamu kwa ajili kuingiza sokoni.
Baada ya kupokea dawa hizo mchungaji Mwamalanga kwa
kushikiana na waumini walishiriki kongamano hilo waliamua kuzitupa chooni
karibu na kanisa hilo alisema kuwa walichukua uamuzi wa kuzitupa chooni bila
kuwa shirikisha Jeshi la polisi kutokana na kukosa imani na jeshi hilo..
No comments:
Post a Comment