Wednesday, June 5, 2013

WANANCHI WILAYA MAKETE WAASWA KUTUNZA MAZINGIRA


Kutoka kushoto ni katibu tawala wilayani Makete Joseph Chota na katikati ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro mwishoni ni Katibu wa ccm wilaya Makete Mraji Mtaturu (picha na riziki bonzuma)

Wananchi wilayani Makete wametakiwa kuhakikisha kuwa wanahifadhi mazingira kwa kuwa ni jambo muhimu ambali litasaidia kuona raha ya kuishi kutokana na mazingira hayo kuzidi kuwa mazuri

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na katibu tawala wilaya hiyo Bw. Joseph Chota katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyoadhimishwa kiwilaya katika kata ya Isapulano



Amesema utunzaji wa mazingira ni jambo zuri na la umuhimu hivyo kuwataka wananchi kutambua umuhimu huo wa kuhifadhi mazingira, ikiwa ni pamoja na kutokata miti ovyo, kutupa taka ovyo pamoja na shughuli zote ambazo zinaharibu mazingira

Matiro amesema ujumbe wa mwaka huu unasisitiza kupunguza matumizi ya rasilimali zisizo rafiki na mazingira pamoja na kupunguza au kuepuka uchafuzi wa mazingira, huku akisistiza kuwa wananchi wakikubali kubadilika mazingira ya makete yatazidi kuwa mazuri siku hadi siku

Kwa upande wao idara ya maliasili wilaya ya Makete imesema jutihada zinaendelea kufanywa na idara hiyo kuhusu utunzaji wa mazingira ambapo wanaendelea kutoa elimu kuhusu kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji pamoja na kupanda miti ambayo ni rafiki na mazingira ikiwemo Mivengi na Mitulunga

Wamesema kwa msimu wa mwaka 2012/2013 zaidi ya miti laki 8 imepandwa wilayani Makete huku lengo la wilaya lilikuwa ni kupanda miti milioni 9 na wameshindwa kupata uhakika kama lengo hilo limefikiwa kutokana na baadhi ya kata 6 ikiwemo Isapulano ambayo maadhimisho hayo yamefanyika, kushindwa kufikisha taarifa za upandaji miti kwenye ofisi ya maliasili na mazingira kwa wakati, ila wanaamini lengo hilo limefikiwa

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani huadhimishwa kila tarehe 5, Juni ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni fikiri kabla ya kula, hifadhi mazingira



Na Eddy blog

No comments:

Post a Comment