Aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Kamuhanda
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP, Saidi Mwema, amemhamishia makao makuu ya jeshi hilo
jijini Dar es Salaam aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Michael
Kamuhanda.
Kamuhanda anakumbukwa kwa kusimamia operesheni
ya jeshi hilo mkoani Iringa dhidi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wakifungua tawi la chama hicho katika kijiji cha
Nyololo Septemba 2 mwaka jana katika operesheni hiyo mwandishi wa habari wa
kituo cha televisheni cha Chanel Ten, Daudi Mwangosi, aliuawa na bomu
lililodaiwa kutoka kwa mmoja wa askari waliokuwa wakimdhibiti mwandishi huyo.
Kutokana na mabadiliko hayo nafasi ya
Kamuhanda imechukuliwa na ACP, Ramadhan Mungi (aliyekuwa Makao Makuu ya
Upelelezi wa Makosa ya Jinai).
Katika taarifa ya Jeshi la Polisi kwa vyombo
vya habari, mbali na Kamuhanda, makamanda wengine waliohamishwa ni ACP Charles
Kenyela (RPC Kinondoni) aliyehamishiwa makao makuu ya upelelezi wa makosa ya
jinai.
DCP, Ally Mlege, aliyekuwa Makao Makuu ya
Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kuwa mkuu wa utawala na
rasilimali watu.
ACP Duwani Nyanda aliyekuwa makao makuu ya
idara ya upelelezi amehamishiwa mkoani Arusha kuwa mkuu wa upelelezi wa makosa
ya jinai.
Taarifa hiyo imeeleza kuwauhamisho huo ni wa
kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment