Wednesday, June 12, 2013

UJENZI WA ZAHANATI YA ITAMBO WANGING'OMBE WAENDELEA SASA BAADA YA KUSIMAMA.

Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe.

Kutokana na Mkataba wa ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Itambo kufanyiwa marekebisho kwa kuongezwa Nyumba ya Mganga ambayo haikuingizwa hapo awali,hatimaye ujenzi huo unatarajia kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumzia hali ya Ujeniz huo Diwani wa Kata ya Mdandu Bi.Annaupendo Gombela amesema kwa kuwa mkataba wa Ujenzi wa Zahanti hiyo ulitakiwa kuisha mwezi julai lakini kutokana na Kuingiza ujenzi wa nyumba ya Mganga kwa pamoja matarajio ni kukamilisha mwezi wa tisa mwaka huu.
Diwani Gombela amesema kuwa hatua iliyofikiwa hadi sasa ni ya ufutaji wa Jamvi katika nyumba na Zahanati hiyo ambapo vinaenda kwa pamoja.
Amesema kuwa pamoja na gharama ya shilingi Milioni Mia Mbili iliyotolewa na Ubalozi wa Japan lakini pia Halmashauri ya Wilaya ya Njombe nayo imeongeza kiasi cha fedha kitakachofanikisha zoezi hilo.
Hata hivyo ameitaka Halmashauri kuwatafuta wataalamu wa Afya mara baada ya Ujenzi kukamilika kwani zoezi hilo litakamilika pamoja na Nyumba za Waganga ikiwa Halmashauri nayo inatarajia kuongeza Nyumba nyingine.
Hadi sasa wananchi wa Kijiji cha Itambo kata ya Mdandu Mkoani Njombe wanatembea Umbali wa Kilomita Nane hadi tisa kwenda kufuata huduma ya Afya katika Kituo cha Afya cha Mdandu na Hivyo kuwasababishia mtatizo mbalimbali katika Maisha yao.

No comments:

Post a Comment