Tuesday, June 11, 2013

WANAICHI WAMKATA MTENDAJI WAO NJOMBE

kiwa umepita mwezi Mmoja tangu wananchi wa Kijiji cha Usuka kumkataa mwenyekiti wao kwa tuhuma mbalimbali hatimaye wananchi wa Kijiji cha Kijombe nao wamemkataa Afisa Mtendaji wao.
Sakata hilo limekuja kufuatia tuhuma zilizokuwa zikimkabili Mtendaji huyo bwana Jailos Lyode pamoja na viongozi wawili wa kamati ya Huduma za Jamii kijijini humo kwa kuhusika na ubadhilifu wa zaidi ya Shilingi Milioni moja ambazo tayari wamezilipa.
 
Akizungumza na Kituo hiki Diwani wa kata ya Kijombe bwana Nashon Kilamlya amesema kuwa Hatua ya wananchi hao kumkata afisa mtendaji huyo imekuja mara baada ya kulipa deni hilo Jana ambalo kwa pamoja walikuwa wakidai shilingi elfu tisini toka zaidi ya shilingi Milioni moja walizolipa hapo
awali.
Diwani Kilamlya amesema ukamilishaji wa deni hilo la shilingi milioni moja Laki mbili na sita elfu limelipwa jana badala ya juni 9 kama ilivyopangwa hapo awali kutokana na Afisa mtendaji huyo kushindwa kuhudhuria mkutano huo kwa siku ya juni 9 mwaka huu.
Kutokana na hali hiyo wananchi hao wakagomea afisa mtendaji huyo kuendelea kufanya kazi katika kijiji hicho na kumtaka aondoke madarakani mara moja hali iliyoulazimu uongozi wa kata kutekeleza agizo la wananchi hao.
Hata hivyo Afisa mtendaji wa kata ya Kijombe ametakiwa kuangalia uwezekano wa kumhamishia katika kijiji kingine ndani ya kata hiyo huku hofu ikiendelea kutanda juu ya Serikali kuendelea tatizo la kuhamishia viongozi wabadhilifu katika maeneo mengine.
Kwa upande wake afisa mtendaji huyo bwana Jailos Lyode amesema kuwa tuhuma hizo hazijamhusu moja kwa moja na kwamba yeye alichohusishwa ni kushindwa kuwasimamia viongozi wa kamati ya Huduma za Jamii na kupelekea kukutwa na tuhuma za kula fedha za Michango ya Msako wa Ukataji ovyo wa misitu na kuchoma mikaa ambao ni uharibifu wa Mazingira.
Aidha amesema kuwa  wananchi hao hawajamkataa bali kuhamishwa kwake kunatokana na maombi aliyoyaomba tangu muda mrefu ambapo leo ameshapata barua toka kwa Afisa mtendaji wa kata ya kuhamia katika kijiji cha Ukomola.

No comments:

Post a Comment