Monday, June 3, 2013

MAJAMBAZI WAUA MMOJA WAJERUHI WAWILI KWA RISASI WAPORA MAMILIONI YA SHILINGI

 Majeruhi wa tukio hilo








WAKATI kikao cha wadau wa ulinzi kinataraji kufanyika kesho jumanne mkoani Iringa katika ukumbi wa Siasa ni kilimo kikao kinacholenga kupambana na mtandao wa uharifu mkoa ya kusini mwa Tanzania ,

Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamevamia maduka eneo la Zizi la Ng'ombe jirani na msikini mjini Iringa na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili kwa risasi kabla ya kupora fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 .

Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na mtandao wa www.matukiodaima.com baada ya kufika eneo la tukio kuwa majambazi hao wakiwa zaidi ya wawili walivamia eneo hilo muda wa saa 1.30 usiku wa leo .

Mashuhuda hao walisema kuwa majambazi hao baada ya kufika katika eneo hilo la kibanda cha M-Pesa kinachomilikiwa na Zamoyoni na kufanikiwa kumpora kiasi hicho cha fedha kabla ya kuelekea katika duka moja wapo maarufu eneo hilo kwa lengo la kuvamia na kupora.

Alisema Kevin Kalinga kuwa chanzo cha kuuwawa kwa mwananchi huyo aliyetambuliwa kwa jina la baba Daudi ni kutokana na kugoma kutii amri ya majambazi hao ambao walimkuta akitoka dukani kununu sigara na kumtaka kukaa chini na baada ya marehemu huyo kugoma kukaa chini ndipo walipomfyatulia risasi mwili jirani na pega na kupelekea kutimua mbio na kujificha chini ya gari lililokuwa limeegeshwa nje ya duka hilo gari aina ya Toyota Hilux lenye namba T 258 .

Hata hivyo baada ya kupigwa risasi kwa mwananchi huyo wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo walianza kujikusanya kwa lengo la kuwavaa majambazi hao hali iliyopelekea majambazi hao kuanza kufyatua risasi ovyo na kujeruhi wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo.

Kwa upande wao majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa wodi namba 5 katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Dismas Nyaulingo ( 20) na Patrick Vatung'a(19) walisema kuwa wao walikuwa wakiendelea kucheza Pool eneo hilo na baada ya kusikia mlio kama wa baruti walianza kujihami kwa kukimbia na ndipo walipokutwa na mkasa huo .


Nyaulingo alisema chanzo cha majambazi hao kuanza kufyatua risasi onyo ovyo ni baada ya wananchi kuanza kujikusanya kwa lengo la kupambana na majambazi hao .

"Sisi tulikuwa tukicheza mchezo wa Pool eneo hilo na baada ya hapo tulisikia mlio wa risasi hewani na tukajua ni baruti na baada ya kusikia mlio wa pili ndipo tulipoanza kutimua mbio kabla ya kupigwa risasi "

Nyaulingo yeye amedai kujeruhiwa eneo la paja lake la mguu wa kushoto huku mwenzake Vatung'a akijeruhiwa eneo la paja la mguu wa kulia.

Madaktari waliowatibu majeruhi hao wamedai kuwa hali zao zinaendelea vizuri na uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi.

Tukio hili limetokea ikiwa ni siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumpandisha cheo aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda ambae kutokana na kupanda kwake kwa cheo wakati wowote kuanzia wiki hii atauaga rasmi mkoa wa Iringa na kwenda kuanza maisha mapya katika kiti cha enzi mpya.

No comments:

Post a Comment