Monday, June 3, 2013

MOURINHO ATAMBULISHWA RASMI NA KUKABIDHIWA UZI WA CHELSEA



YAMETIMIA. Jose Mourinho amesaini Mkataba wa miaka minne na kupewa rasmi mikoba ya kufundisha tena Chelsea.
hatimaye saa kadhaa baadaye Mourinho anazungumza kwa furaha akijitambulisha kama kocha mpya wa Chelsea.
Alipoulizwa juu ya kuifanya Chelsea iwe bora, Mourinho alijibu: "Hakika ni ujumbe ule ule, lakini sasa naweza kusema mimi ni mmoja wenu na hiyo ni tofauti.
"Haijawahi kutokea maishani mwangu kwenye soka nikavutiwa na timu kama Inter na Chelsea. Na Chelsea ni zaidi ya muhimu kwangu. Ilikuwa ngumu ngumu sana kucheza dhidi ya Chelsea na nilifanya hivi mara mbili tu ambayo haikuwa mbaya sana. Hakika naahidi kitu kile kile nilichoahidi mwaka 2004 na tofauti ya kwamba mimi. Ni ambaye ni miongoni mwenu,"alisema Mourinho ambaye atatambulishwa rasmi katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jumatatu ya Juni 10.

Mourinho ametua na benchi lake la ufundi linaloundwa na Rui Faria, Silvino Louro na Jose Morais aliokuwa nao Real, na yu tayari kujipanga kuipa Chelsea taji la kwanza la Ligi Kuu ya England msimu ujao tangu mwaka 2010.
Taarifa katika tovuti ya klabu hiyo imesema: "Klabu ya soka ya Chelsea inayo furaha kutangaza kuteuliwa kwa Jose Mourinho kama Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza.
Mourinho amesaini Mkataba wa miaka minne na atarejea katika klabu ambayo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England, Kombe la FA na mawili ya Kombe la Ligikati ya mwaka 2004 na 2007.
Ametua na wasaidizi wake katika benchi la ufundi ambao ni Rui Faria, Silvino Louro na Jose Morais, ambao watafanya kazi pamoja na benchi la ufundi la sasa la timu ya kwanza, Steve Holland, Christophe Lollichon na Chris Jones,"ilisema taarifa ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment