Monday, June 3, 2013

JESHI LA POLISI MKOANI NJOMBE LAFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI


Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limewataka Viongozi wa Dini Kuendelea Kudumisha Amani na Utulivu na Kukemea Migogoro ya Kidini Katika Nyumba za Ibada Pamoja na Kuwataja Watu Wanaochochea Chuki za Kidini Miongoni Mwa Watanzania.

Aidha Jeshi Hilo Pia Limewataka Waumini Kuacha Kujihusisha na Mambo ya Kisiasa Katika Masuala ya Kidini Kwani Kwa Kufanya Hivyo Itazidi Kuchochea Machafuko ya Kidini Jambo Linaloweza Kuhatarisha Amani ya Nchi na Utulivu Uliopo.

Akizungumza na Viongozi wa Dini Mjini Njombe Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani Amesema Lengo la Kuwakutanisha Viongozi Hao ni Kwaajili ya Kutambua Nafasi ya Viongozi wa Dini Katika Kutunza na Kulinda Amani ya Nchi.

Amesema Viongozi wa Dini Wana Nafasi Kubwa Katika Kuelimisha Waumini na Jamii Kuhusu Athari na Namna ya Kuhepuka Migogoro ya Kidini na Mivutano ya Kisiasa na Kusema Kuwa Ushirikiano Kati ya Jeshi la Polisi na Viongozi Hao ni Nguzo Imara Katika Kukabiliana na Migogoro Hiyo.

Aidha Kamanda Ngonyani Pia Amekemea Tabia ya Baadhi ya Askari Wanaotoa Taarifa za Siri Juu ya Taarifa za Uhalifu Zinazowasilishwa Kwa Jeshi Hilo Kutoka Kwa Raia Wema

Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Baadhi ya Viongozi wa Dini Waliohudhuria Mkutano Huo Wameliomba Jeshi la Polisi Kuchukua Hatua Dhidi ya Matukio ya Uhalifu na Ubakaji Yanayojitokeza Kwasasa Mkoani Hapa

Kwa upande Wake mrakibu msaidizi wa polisi Focas Malengo na maafisa upelelezi mkoa wa Njombe wakasemaushirikiano ni wa muhimu katika jamii ikiwemo kutoa taarifa za uharifu iwe kwa vikosi vya jeshi la polisi ama mwananchi yeyote anaekwenda kinyume na matakwa ya umma pamoja na kuwataja wale wote wanaohusika kukosesha jamii kwa kuwaibia,mauaji,ubakaji na udokozi.

Mkutano Huo Ulilenga Kuzungumzia Namna ya Ushiriki wa Viongozi wa Dini Katika Kutunza na Kulinda Amani Iliopo Kwasasa Hapa Nchini Ambayo Imeanza Kutetereka Kutokana na Kuanza Kujitokeza Kwa Itikadi za Kidini Miongoni Mwa Watanzania

NA MICHAEL NGILANGWA

No comments:

Post a Comment