Wednesday, June 19, 2013

HILI NI BARAA JAMANI

Mwalimu wa masomo ya ziada ( tuition) katika kituo  cha itunge  wilayani kyela  anashikiriwa na jeshi la polisi mkoani mbeya kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi DIWANI ATHUMANI amesema tukio hilo limetokea juni 17 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni eneo la kijiji cha itunge wilaya ya kyela.

IPYANA GIDION (30) amembaka mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi mbugani  miaka 10 na kumsababishia maumivu makali mwilini.
ATHUMANI amesema  mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha kuondoka na kubaki na mhanga huyo DARASANI
Amesema mtuhumiwa huyo ambaye amewahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka kwa rufaa amekamatwa na taratibu za kumpeleka mahakamani zinafuatwa
 Athumani ametoa wito kwa jamii kuacha tamaa za mwili badala yake kuwa waaminifu katika majukumu ambayo wamepewa dhamana na jamii ili kuyatekeleza kwa uadilifu

No comments:

Post a Comment